Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KITAIFA , HABARI ZA LEO - Tanzania kinara huduma bora Afrika

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
UMOJA wa Mataifa (UN), umeitangaza Tanzania kuwa mshindi katika utoaji wa huduma bora za utumishi wa umma kwa jamii barani Afrika, katika maadhimisho wa Wiki ya Utumishi wa Umma, yaliyohitimishwa jana.


Tanzania ilipata ushindi huo kupitia Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) na kukabidhiwa tuzo yake jana katika Viwanja vya Mnazi mmoja, jijini Dar es Salaam.


Makamu wa Rais Dk Gharib Mohamed Bilal na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wassira. waliiwakilisha serikali katika hafla ya kuhitimisha maadhimisho hayo ya kimataifa yaliyofanyika nchini kwa mara ya kwanza.


Akizungumza na Mwananchi baada ya kupokea tuzo hiyo, waziri Wassira alisema tuzo hiyo imeleta furaha kwa taifa na kwamba hayo ni matokeo ya ushirikishwaji wa wananchi katika mipango na mikakati ya serikali katika kuleta maendeleo.


Alisema tuzo hiyo imetolewa baada ya serikali kupitia mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (Mkurabita), kufanya vizuri na kuleta mabadiliko ya kiuchumi kwa wananchi.


Wassira alisema tuzo hiyo imetokana na utekelezaji wa kauli mbiu ya Wiki ya Utumishi Afrika isemayo ‘Mabadiliko na Ubunifu katika Uongozi na Utumishi wa Umma yanaleta maisha bora kwa kila mtu’. “Uongozi mzuri uliowashirikisha wananchi katika Mkurabita umepokelewa vizuri na kuzaa matunda iliyowezesha kupata tuzo hii ya kimataifa," ’alisema Wassira.


Waziri huyo alizitaka halmashauri kuwa na mipango inayoleta maendeleo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa wananchi wanapata hati miliki za ardhi.


Wassira alisema ukosefu wa hati hizo, ndio chanzo cha umaskini miongoni mwa wananchi katika nchi za Afrika ikiwamo Tanzania na kwamba kuna haja ya kushughulikia tatizo hilo.Tanzania imeshika nafasi ya kwanza barani Afrika katika kipengele cha pili cha kuwania tuzo kuhusu utoaji wa huduma bora za utumishi wa umma.


Nchi nyingine zilizoshika nafasi ya kwanza ni India, Poland, Columbia na Oman wakati zilizoshika nafasi ya pili ni Tunisia, Korea, Uholanzi na Peru.Nchi zilizoshinda katika kipengele cha kwanza kuhusu kuzuia na kupambana na rushwa katika utumishi wa umma kinara ni Korea ,Slovakia, Mexico na Oman wakati nafasi ya pili imechukuliwa na Romania ,Afrika Kusini na Misri.

0 comments

Post a Comment