IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
CHAMA cha NCCR-Mageuzi kimesema kuwa tayari kimeandaa barua ambazo kitaziwasilisha kwa Waziri wa Fedha, Bw. Mustafa Mkulo kuelekeza posho za
vikao kwa wabunge wanne wa chama hicho zipelekwe kwenye miradi ya maendeleo kwa Mkoa wa Kogoma.
Mkuu wa Idara ya Habari na Uenezi wa chama hicho, Bw. David Kafulila alisema hayo jana kuhusu Bajeti ya mwaka 2011, 2012 na kubainisha mambo mbalimbali juu ya ukuaji wa uchumi, deni la taifa, misaada na mikopo na suala zima la vipaumbele katika uchumi wa nchi.
Msimamo huo wa NCCR-Mageuzi unaunga mkono hoja ya Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni inayoongozwa na CHADEMA ambayo tayari imeweka msimamo huo, huku Waziri Kivuli wa Fedha, Bw. Zitto Kabwe akienda mbali zaidi kwa kuwasilisha barua ofisi ya bunge kutaka posho zake za vikao zipelekwe kwenye taasisi ya Kigoma Development Initiative (KDI).
Bw. Kafulila alisema kuwa mbali na kupendekeza posho zao kuelekeza kwenye miradi ya maendeleo, pia wanapendekeza posho zote zikatwe kodi ili kuongeza mapato ya ndani kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Mbunge huyo alisema kuwa barua hiy leo itapelekwa kwa Waziri wa Fedha na nakala yake kwa Sipka wa Bunge, wakiwataka fedha zao za vikao vya bunge zipelekwe kwenye kifungu74 ambalo ni fungu la miradi ya maendeleo kwa Mkoa wa Kigoma.
"Uamuzi huu pia tumeamua kuufanya kwa kuwa moja ya sehemu kubwa ya mapato hutumika kushibisha mfumo mkubwa na udhaifu wa kiutawala pamoja na ufisadi, hata ukiangalia katika serikali kuna vyeo vingi kwa mfano hiki cha ukuu wa wilaya kina kazi gani, watu wanakula fedha na kazi hawafanyi huu ni mlundikano wa madaraka kwa watu ambao hawana hata kazi," alisema.
Alisema kuwa wao kama chama cha upinzani wataendelea kusisitiza mabadiliko ya mfumo wa utawala katika eneo moja tu la kuondoa wakuu wa wilaya na makatibu tarafa nchini na kubaki na uongozi wa halamshauri ambao unatosha kusimamia majukumu yote ya ndani ya wilaya na kuokoa fedha ambazo zinatosha kununulia mitambo mipya yenye uwezo wa kuzalisha umeme zaidi ya megawati 200.
You Are Here: Home - HABARI ZA KITAIFA , HABARI ZA LEO - POSHO ZA VIKAO: NCCR yaunga mkono CHADEMA
0 comments