Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KITAIFA , HABARI ZA LEO - Mpendazoe awakaanga Sitta, Mwakyembe

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Kushoto ni Fred Mpendazoe, katikati John Shibuda na kulia, ni Bob Makani 
KADA maarufu wa Chadema, Fred Mpendazoe amezindua kitabu kinachobainisha harakati za ukombozi mpya wa nchi, huku akiendelea kuwaandama makada maarufu wa CCM wakiwamo Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mshariki, Samuel Sitta na Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harison Mwakyembe.


Kitabu hicho kilizinduliwa jana na Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lisu katika kongamano la vijana wa Chadema kuhusu katiba lililofanyika katika ukumbi wa Polisi Jamii mjini Dodoma.


Kitabu hicho kiitwacho "TUTASHINDA", pamoja na mambo mengine, kinazungumzia harakati za Mpendazoe katika utumishi wake kwa umma na harakati za kisiasa za kada huyo wa Chadema ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa CCM katika Jimbo la Kishapu kuanzia Desemba 2005 hadi alipojiondoa katika chama hicho Machi 30, 2010 siku chache kabla ya kuvunjwa kwa bunge la tisa.


Mbali na Sitta na Mwakyembe pia kitabu hicho kinawataja Mbunge wa Lupa, Victor Mwambalaswa, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye na kada wa CCM, Daniel Porokwa kuwa miongoni mwa waanzilishi wa kilichokuwa Chama cha Jamii (CCJ) na kwamba watu hao ni wasaliti wasiostahili kuaminiwa na Watanzania katika vita dhidi ya ufisadi.


Akizumgumza mara baada ya uzinduzi huo, Mpendazoe alisema huu ni wakati wa kutafuta upya uhuru wa Taifa kutokana na ukweli kwamba hivi sasa nchi iko njia panda kwani hakuna matumaini.
"Ni miaka 50 ya tangu tupate uhuru lakini ukweli ni kwamba nchi yetu iko njiapanda, ni wakati wa kutafuta upya uhuru wa nchi yetu na kuagalia ni kipi cha kufanya ili kulitenga taifa letu la Tanzania,"alisema Mpendazoe na kuongea:
"Jina hili la kitabu 'tutashinda' linamaanisha kwamba baada ya kufanya tathimini ya harakati za vita dhidi ya ufisadi vinavyofanywa na wadau mbalimbali wakiwemo chama chetu cha Chadema, wasomi, wanasiasa na wanaharakati nimefikia hitimisho kwamba ushindi upo, yaani tutashinda".


Alisema uzoefu alioupata katika mchakato wakuendesha CCJ unathibitisha kwamba Mwakyembe na Sitta walimsaliti na kumwacha njia panda akiwa peke yake baada ya kuwa wameahidiwa vyeo vipya ndni ya CCM ambayo awali walikuwa wameamua kuipa kisogo.


Alisema kutokana na hilo viongozi hao ni 'wapambanaji feki' wasiostahili kuaminiwa tena na katika mapambano dhidi ya ufisadi nchini.Kwa mujibu wa Mpendazoe lasima yafanyike mageuzi ya kimfumo katika uendeshaji wa nchi na kwamba "Nguvu ya upendo itakapoishinda tamaa ya madaraka, ndipo dunia itakapopata amani".


Kitabu hicho chenye sura kumi na moja, pia kinazungumzia katiba mpya na umuhimu wa kuwa na Tume huru ya Uchaguzi kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2015 na kwamba katika imani hakuna chochote kisichowezekana.


Maudhui ya Kitabu
Miongoni mwa maudhui ya kitabi cha TUTASHINDA ni uchambuzi kuhusu historia ya nchi ambapo anabainisha kuwa tofauti na enzi za uongozi wa hayati Mwalimu Nyerere, hivi sasa viongozi hawaheshimu katiba, utawala wa sheria wala viapo vyao vya kiuongozi.


Kadhalika Mpendazoe anataja tatizo la rushwa kuwa kiini cha matatizo mengi yanayolikabili taifa na kwamba kushindwa kuondoka kwa tatio hilo ni matokeo ya mmomonyoko wa maadili ya viongozi ambao wamekuwa sehemu ya uonzo huo


Kuhusu CCJ, Mpendazoe aliyataja majukumu waliyopeana wakati wa mchakato wa kuanzisha CCJ kuwa Nnape alipewa jukumu la kuandika katiba, Mwakyembe alishiriki kuandaa nyaraka za kisheria zilizokuwa zikihitajikma kwa ajili ya usajili na Sitta alikuwa na wajibu wa kutafuta fedha za uendeshaji wa chama hicho.


Kadhalika amezungumzia kujivua gamba kwa CCM alisema kama kweli chama kitawaondoa watuhumiwa wote wa ufisadi ndani ya siku 90 kama ambavyo chama hicho kimekuwa kikiahidi basi hakuna atakayesalimika na kwamba Watanzania wategemee kuitishwa kwa uchaguzi mkuu kabla ya 2015.

0 comments

Post a Comment