Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KIMATAIFA , HABARI ZA LEO - Benki ya Dunia yamwaga fedha Tanzania

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
BENKI ya Dunia (WB) imeanzisha mkakati mpya wa kuisaidia Tanzania utakaoipatia zaidi ya dola za Marekani bilioni 2.8 kutoka Jumuiya ya Misaada ya Kimataifa (IDA), kwa miaka minne kuanzia 2012 hadi 2015.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Benki hiyo kwa Tanzania, Uganda na Burundi, John Mclntire, fedha hizo ambazo ni sawa na zaidi ya Sh trilioni nne, zitatolewa kwa ajili ya kuendeleza maeneo yaliyoainishwa kuwa vipaumbele muhimu na nchi husika bila kuwepo masharti mengine.

Wakati akieleza kuhusu mkakati huo mpya Dar es Salaam jana, Mclntire alisema vipaumbele hivyo ni vilivyoainishwa katika Mpango waTaifa wa Kukuza Uchumi na Kuondoa Umasikini (MKUKUTA II) kwa Tanzania Bara, na Mpango wa Kukuza Uchumi na kuondoa Umasikini Zanzibar (MKUZA II).

Mclntire alisema, WB katika mpango wake wa kukuza uhusiano na Tanzania, itaendelea kujikita katika kuisaidia na kuhakikisha inafanikiwa kupanua uchumi, kujilinda na kuhimili vishindo vya mitikisiko ya kiuchumi inayotokana na sababu mbalimbali.

Alisema,“WB inatambua changamoto zinazoikabili Tanzania kutokana na miundombinu duni iliyonayo. Inatambua pia tatizo kubwa la mitaji linaloikabili katika kukuza uchumi wake na hivyo kuona umuhimu wa kuhakikisha inazikabili kwa kuielekezea misaada na mikopo nafuu”.

Pamoja na hayo, alisema benki hiyo itahakikisha maeneo muhimu kama ujenzi wa miundombinu imara, uendelezaji na uimarishaji wa maeneo ya kibiashara, kilimo chenye ufanisi, ujenzi wa uwezo wa kiutendaji wa wafanyakazi katika maeneo ya uzalishaji na uendelezaji wa mipango miji inatengewa kiasi cha kutosha kutoka katika misaada hiyo.

“Hiyo ndiyo njia pekee tunayoweza kuhakikisha Tanzania inakabili changamoto hizo kutokana na mikopo na misaada inayopewa kutoka katika benki yetu,”aliongeza.

Aidha alitaja madhumuni mengine ya mkakati huo mpya kuwa ni kukuza na kuendeleza mazingira bora kwa sekta binafsi kushiriki kukuza uchumi wa nchi, utawala bora na uwajibikaji kwa wenye dhamana ya Maendeleo ya uchumi wa nchi.

0 comments

Post a Comment