Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KITAIFA , HABARI ZA LEO - BAJETI 2011/2012: Wabunge wagawanyika

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Bajeti ya Serikali kama ilivyosomwa na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustapha Mkulo (pichani) Jumatano iliyopita, imegawa mapokeo ya wabunge, baadhi wakisifia wengine wakiiponda.

Wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) walisifu kwamba imezingatia kilio cha wananchi, wakati wale wa upinzani waliikosoa kuwa bado ina matatizo mengi.

Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe aliye Mbunge wa Hai (Chadema), alisema kuwa bajeti haina ubaya wa moja kwa moja lakini kasoro nyingi zitajionesha wakati wa utekelezaji wa wizara.

Mbunge wa Wawi (CUF), Hamad Rashid alisema kuwa serikali haijawa sikivu katika hoja za msingi kiasi kwamba bajeti imeshindwa kuzungumzia kiwanda cha ngano ambacho kipo tayari.

Alisema kuwa mpaka leo bado serikali inaagiza ngano kutoka nje ya nchi, huku misamaha ya kodi kwenye sekta ya madini ikizidi kutesa mapato ya nchi.

Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Haruna Lipumba alisema kuwa bajeti bado ina matatizo makubwa kwa sababu mwanzo mpaka mwisho, Mkullo hakueleza pato la serikali katika sekta ya madini.

Alisema, bado kuna misamaha ya kodi isiyo na maslahi kwa nchi na kuongeza kwamba bajeti ya mwaka huu imekwenda kinyume na ahadi ya serikali iliyoweka kwenye Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).

Zitto akizungumza na gazeti hili kwa simu alisema: “Kuna mambo ambayo serikali imefuata mapendekezo yetu. Kupunguza posho za watumishi wa serikali ambayo ni kilio changu siku zote na utatuzi wa kero za wanafunzi wa elimu ya juu lakini kwenye madini hakuna hatua ya maana ambayo serikali imechukua.”

Kwa upande mwingine, Waziri wa Ardhi na Makazi, Anna Tibaijuka na wabunge wa CCM, Amina Nassor Mwakilagi, Martha Mlata, Sara Msafiri na Ahamed Shabiby ‘waliifagilia’ bajeti kwamba itamkomboa Mtanzania.Bajeti ya Serikali kama ilivyosomwa na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustapha Mkullo (pichani) Jumatano iliyopita, imegawa mapokeo ya wabunge, baadhi wakisifia wengine wakiiponda.

Wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) walisifu kwamba imezingatia kilio cha wananchi, wakati wale wa upinzani waliikosoa kuwa bado ina matatizo mengi.

Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe aliye Mbunge wa Hai (Chadema), alisema kuwa bajeti haina ubaya wa moja kwa moja lakini kasoro nyingi zitajionesha wakati wa utekelezaji wa wizara.

Mbunge wa Wawi (CUF), Hamad Rashid alisema kuwa serikali haijawa sikivu katika hoja za msingi kiasi kwamba bajeti imeshindwa kuzungumzia kiwanda cha ngano ambacho kipo tayari.

Alisema kuwa mpaka leo bado serikali inaagiza ngano kutoka nje ya nchi, huku misamaha ya kodi kwenye sekta ya madini ikizidi kutesa mapato ya nchi.

Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Haruna Lipumba alisema kuwa bajeti bado ina matatizo makubwa kwa sababu mwanzo mpaka mwisho, Mkullo hakueleza pato la serikali katika sekta ya madini.

Alisema, bado kuna misamaha ya kodi isiyo na maslahi kwa nchi na kuongeza kwamba bajeti ya mwaka huu imekwenda kinyume na ahadi ya serikali iliyoweka kwenye Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).

Zitto akizungumza na gazeti hili kwa simu alisema: “Kuna mambo ambayo serikali imefuata mapendekezo yetu. Kupunguza posho za watumishi wa serikali ambayo ni kilio changu siku zote na utatuzi wa kero za wanafunzi wa elimu ya juu lakini kwenye madini hakuna hatua ya maana ambayo serikali imechukua.”

Kwa upande mwingine, Waziri wa Ardhi na Makazi, Anna Tibaijuka na wabunge wa CCM, Amina Nassor Mwakilagi, Martha Mlata, Sara Msafiri na Ahamed Shabiby ‘waliifagilia’ bajeti kwamba itamkomboa Mtanzania.

0 comments

Post a Comment