Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KISIASA , HABARI ZA KITAIFA , HABARI ZA LEO - Uongozi wa Spika Makinda wadaiwa kusababisha mpasuko ofisi za Bunge

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
BAADHI ya wafanyakazi wa Ofisi ya Bunge wametoa tuhuma nzito kwa baadhi ya viongozi wao wa juu kutokana na kile wanachokiita ni kubaguliwa kwa kuitwa ni watu wa kundi la Spika mstaafu Samuel Sitta.

Wakizungumza Dares Salaam jana kwa sharti la kutotajwa, watumishi hao ambao ni waathirika wa ubaguzi huo, walisema kitendo hicho ni ubaguzi unaodhoofisha ufanisi uliokuwa umefikiwa na uongozi wa Bunge uliopita.

Kwa mujibu wa watumishi hao, hatua hiyo imekuwa ikitokana na hofu ya kufichuka maovu na udhaifu wa utendaji na kuvuja kwa jamii ndiyo maana, kuna watu wanaitwa, "hawa wa Sitta."

Mmoja wa wafanyakazi hao alifafanua zaidi kwamba, hata Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashillilah, ingawa ni mteule wa rais, lakini naye amekuwa akibaguliwa akiitwa mtu wa Sitta na kuna kipindi alifikia hatua ya kutaka kujiuzulu.
Lakini, Dk Kashilila ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya Bunge, alipoulizwa kwa simu jana, alisema: "Acha nifanye uchunguzi kuona kama kuna kitu hicho."

Dk Kashillilah alisema jambo kama hilo anapaswa kuwasiliana na idara mbalimbali za Bunge na kusisitiza: "Nikianza kuzungumza bila kushirikisha wenzangu ambao labda wanajua vyema sitakutendea haki wewe na mimi pia."

Aliongeza kuwa hadi sasa yeye hajapata malalamiko hayo mezani kwake na kwamba, labda yatakuwa pembeni.
Alisema hadi sasa hakuna ajira mpya ambazo Bunge limefanya na kusisitiza, kama wapo miongoni mwa waliopo wanabaguliwa kwa msingi huo, atajaribu kulifuatilia na wenzake kuona ukweli wake.

Alipoulizwa kwamba yeye ni mmoja waathirika hao wanaoitwa 'watu wa Sitta na alikuwa akitaka kuachia ngazi kutokana na majungu hayo,' alicheka kisha akasema: "Hilo mimi silijui."

Mtendaji mkuu huyo wa bunge alisema wafanyakazi hao waliendelea kuhoji aina hiyo ya uongozi wa kubagua watu wakati spika aliyepita alimrithi hadi katibu wa bunge.Kwa mujibu wa wafanyakazi hao, kutokana na kuajiriwa baadhi ya watu wakiwamo madereva wasiokuwa na sifa, kumesababisha hata gari aina ya Mercedes Benz iliyokuwa ya Spika kupata ajali, baada ya dereva wake kugonga gari kwa nyuma.

Walidai kuwa baadhi yao wamekuwa wakifika ofisini bila kupangiwa kazi, hali ambayo inawaathiri kisaikolojia.

0 comments

Post a Comment