IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
Kiongozi wa Sudan Kusini Salva Kiir amesema hatawaongoza watu wake kwenye vita na Kaskazini kuhusu eneo lenye mgogoro la Abyei.
Eneo la Abyei lilichukuliwa na vikosi vya Kaskazini mwishoni mwa wiki,liko kwenye mgogoro na Kusini ambayo inatarajia kutengana na Kaskazini na kuwa huru kuanzia Julai mwaka huu.
"Hatutarudi vitani tena, haitatokea," Bwana Kiir alisema katika taarifa yake ya kwanza kwa umma tangu tatizo la Abyei ianze.
Wachambuzi wanahofia kuwa mgogoro huo utaanzisha mapigano tena kati ya Kusini na Kaskazini.
Makubaliano ya amani ya mwaka 2005 yalimaliza miaka 22 ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyosababisha watu milioni 1.5 kufa.
Uamuzi kuhusu eneo la Abyei haukutolewa na rasimu yake iliyokuwa ikamilike mwezi Januari kujua iwapo eneo hilo liwe limilikiwe na Kaskazini au Kusini imeahirishwa na haijulikani itakamilika lini.
Katika hotuba yake kwa Taifa, Bwana Kiir alisema Kusini imepigana vita vya kutosha na kwamba sasa ni wakati wa amani.
Ameuelezea uvamizi wa Kaskazini kwenye eneo la Abyei kama ni 'kuhamaki' na kuongeza kuwa eneo hilo hatimaye litarudi Kusini.
Rais wa Sudan Omar al-Bashir amekataa kuondoa vikosi vyake katika eneo la Abyei licha ya Umoja wa Mataifa kushutumu uvamizi huo.
Awali, waziri wa serikali ya Kitaifa anayetoka Kusini alijiuzulu akisema 'uhalifu wa kivita' umefanyika katika eneo hilo la Abyei.
You Are Here: Home - HABARI ZA KIMATAIFA , HABARI ZA KITAIFA , HABARI ZA LEO - Sudan Kusini ' haitoingia vitani'
0 comments