ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Chama cha Jamii (CCJ), Richard Kiyabo amekanusha kuwa wanachama watatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samuel Sitta, Dk. Harrison Mwakyembe na Nape Nnauye, walikuwa waasisi wa chama hicho cha upinzani.
Pia amekitaka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kuacha kufanya siasa za udaku na kusema uongo na badala yake kijikite kutangaza sera zake kwa manufaa ya taifa.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Kiyabo alisema, akiwa kama Mwenyekiti wa CCJ kilichopewa usajili wa muda Machi mwaka jana, anafahamu kuwa waanzishili wa chama hicho ni wawili.
“Mimi na mwenzangu ambaye alikuwa Katibu Mkuu, Renatus Muabhi ndio viongozi waanzilishi wa CCJ, wengine tuliwaomba ushauri tu wa kawaida na ni watu tofauti wakiwamo wasomi, waandishi wa habari, wanasiasa na hata wanafunzi wa vyuo vikuu,” alisema Kiyabo.
Amesema, wakati chama hicho kikianzishwa, baadhi ya watu waliojiunga ni pamoja na aliyekuwa Mbunge Kishapu kupitia CCM, Fred Mpendazoe.
“Alipopata nafasi hii (Mpendazoe) alikurupuka na kuacha jimbo lake, chama chake, mke wake na kuingia CCJ ambako alitaka pia kuwa Mwenyekiti, tukaamua kumpa wadhifa wa msemaji wa chama,” amesema Kiyabo.
Amesema, inashangaza na kusikitisha kusikia Mpendazoe hivi karibuni akiudanganya umma kuwa Nape ambaye ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Sitta anayeongoza Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Naibu Waziri wa Ujenzi Dk. Mwakyembe na Mbunge wa Lupa, Victor Mwambalaswa ni waanzilishi wa CCJ jambo ambalo si kweli.
“Kwa kweli katika kuanzisha CCJ, watu hawa siwatambui na hata huyo Mpendazoe mwenyewe alikuwa mgeni kwenye chama hicho,” alisema.
Alitaka Mpendazoe aulizwe kama kweli madai yake kuwa viongozi hao ni waanzilishi wa CCJ, je wakati alipojiunga na chama hicho, nani alimpokea na ilikuaje hadi akakaririwa na vyombo vya habari akimkaribisha Sitta CCJ wakati kwa madai yake tayari kiongozi huyo ni muasisi wa chama hicho.
Kwa mujibu wa Kyabo, kuanzia uamuzi wa chama na hata nyaraka hadi chama hicho kinafutwa, saini na kila kitu kilikuwa chini ya Kiyabo na Muabhi.
Alisema wakati umefika kwa Chadema kuacha siasa za udaku kwa kuwa hazitowafikisha Ikulu.
“Watambue kuwa Watanzania wa sasa ni waelewa sana ndiyo maana nawashauri wajikite kwenye kutangaza sera za chama, wakiendelea hivyo tutakuwa na imani kuwa udaku ndio sera yao mpya.
Amekitaka chama hicho kuzungumzia mustakabali wa taifa na kuacha kuhamasisha maandamano na vurugu ya kutaka kuingia madarakani kupitia nguvu ya umma badala ya demokrasia ya kura.
Katibu Mkuu wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, Dk. Kilumbe Ng’enda, alikitaka Chadema kujibu hoja za Nape kuhusu ufisadi unaoendelea ndani ya chama hicho akitolea mfano mshahara wa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa badala ya kuanzisha hoja za uongo kukwepesha ukweli.
Amesema, chama hicho kimemshutumu Nape kuwa anakirushia madongo kwa sasa baada ya kukataliwa kugombea Chadema wakati wa Uchaguzi Mkuu ambapo alianguka katika kura za maoni alipowania nafasi ya Ubunge Jimbo la Ubungo.
“Huu ni uongo mtupu, Nape hajawahi kugombea Chadema, asingekuwa na nguvu ya kuanika ufisadi wa chama hicho kama vile ubinafsi na ukabila"
Alisema ukabila na ubinafsi wa Chadema ulioonekana katika nafasi za Viti Maalumu ambapo Mkoa wa Kilimanjaro, uliotoa wabunge wengi wa viti maalumu kuliko mikoa mingine yenye kura nyingi na sasa mshahara wa Dk. Slaa ambao ni Sh milioni 7.5 kwa mwezi kuuzidi wa Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama ambao ni Sh milioni 1.5 kwa mwezi.
“Maneno yanayotoka mdomoni mwa viongozi wa Chadema hayafanani na matendo yao, wakati Dk. Slaa anapata kiasi hicho cha fedha, makatibu wa chama hicho wa wilaya wanapoteza virutubisho mwilini mwao kwa maandamano, Chadema na wao wajivue gamba la ukabila na ubinafsi,” alisema Kyabo.

0 comments