Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KITAIFA , HABARI ZA LEO - Mwakyembe atoa siku tano kupata vielelezo

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
NAIBU Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe ametoa siku tano kuchunguzwa kwa mkandarasi wa Kampuni ya Ujenzi ya Y.N Investment and Lucky Construction ambaye alipewa kukarabati barabara ya kutoka Muheza mjini Kwenda Amani kwa madai ya kwenda kinyume na mkataba.


Mwakyembe alitoa kauli hiyo baada ya kukagua barabara hiyo akiwa katika ziara wilaya humu.Awali katika taarifa yao kwake, viongozi wa wilaya walimweleza Naibu Waziri kuwa hawaridhishwi na mkandarasi huyo kwani tangu apewe tenda hiyo hajafanya chochote katika barabara hiyo.


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza, Amiri Kiroboto alisema mkandarasi huyo alipewa tenda ya kukarabati barabara hiyo tangu mwaka 2009, lakini mpaka sasa imefika miaka miwili hajakarabati kabisa.


Alisema kuwa mkandarasi huyo alipewa tenda hiyo ya kukarabati barabara kwa muda wa miaka mitano kutoka Tanga mjini mpaka Wilaya ya Pangani kwenda Wilaya ya Muheza kutoka Muheza mpaka Amani kwa gharama ya Sh 3.5 bilioni .


Alisema mpaka sasa alishapokea Sh 616 milioni na bado anadai Sh 2.9 bilioni anazotakiwa kulipwa kadri anavyotekeleza mkataba.


Naye Mbunge wa Jimbo la Muheza, Herbert Mntangi alisema katika vikao vya mkoa vikiwemo RCC na vya Bodi ya barabara ya mkoa walishapitisha azimio la kumkataa mkandarasi huyo.


Kufuatia kauli hizo, Naibu Waziri wa Ujenzi aliamua papo kwa papo kutembelea barabara hiyo kujionea mwenyewe udhaifu wa mkandarasi huyo.


Katika majumuisho ya ziara hiyo, Mwakyembe alitoa siku tano kwa viongozi wa wilaya na mkoa kukusanya na kuwasilisha vielelezo vyote vya vikao vilivyomkataa mkandarasi huyo apewe Meneja wa Tanroad Mkoa wa Tanga, Alfred Ndumbalo ambaye atavipeleka kwake.

0 comments

Post a Comment