Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KITAIFA , HABARI ZA LEO - Miili yatelekezwa barabarani Tarime

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter Umekuwepo mkanganyiko mkubwa baina ya wafiwa, serikali na wanaharakati Kufuatia mauaji ya watu kadhaa waliouawa na askari polisi kwa kupigwa risasi wakituhumiwa kutaka kupora Mgodi wa African Barrick North uliopop katika eneo la Nyamongo, Wilaya ya Tarime, mkoani Mara, Tanzania.


Mkanganyiko huo wa ama maiti zizikwe au la, ili kupisha uchunguzi, umesababisha mtafaruku ambao umewaacha maiti hao wakiwa wametelekezwa mitaani, vile vile, baadhi ya wanaharakati na viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, wamekamatwa kuhusiana na tukio hili.


Pichani ni ndugu na jamaa wakiwa wamepigwa butwaa wasijue la kufanya baada ya maiti ya Chawali Bhoke na wengine ikiwa imetelekezwa mitaani katika vijiji vya Bonchugu wilayani Serengeti leo hii.

0 comments

Post a Comment