MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, mkoani Mbeya, John Mwankenja ameuawa kwa kupigwa risasi kichwani na watu wasiojukana, usiku wa kuamkia jana katika eneo la nyumbani kwake.
Mmoja wa watu wa karibu na marehemu, Bahati Lupumbwe alisema Mwankenja ambaye pia alikuwa Diwani wa Kiwira, aliuawa wakati akijiandaa kuegesha gari lake.
Alisema mauaji hayo yamefanywa na kundi la watu watatu waliokuwa wamefunika sura zao kwa kutumia vitambaa vyeusi na kumwamuru marehemu kulala chini na baadaye, kumshambulia kwa risasi kichwani.
Lupumwe alisema baada ya mauaji hayo ya kinyama, watu hao walitokomea kusikojulikana na habari zilisema hakuna walichokichukua kutoka nyumbani kwa marehemu.
Mdogo wa marehemu, Alinanuswe Mwankenja, alisema kifo cha kaka yake kimeleta mshituko mkubwa katika ukoo wao hasa ikizinagiwa kuwa saa kadhaa kabla ya kuuawa kwake, aliaga kuwa alikuwa anakwenda kumwona mke wake, aliyelazwa katika Hospitali ya Meta, jijini Mbeya.
Kwa upande wake, Mbunge wa Viti Maalumu mkoani Mbeya, Hilda Ngoye, alielezea kusikitishwa kwake juu ya mauaji ya kiongozi huyo wa halmashauri.
Alisema Mwankenja ameacha pengo kubwa katika familia yake, ndani ya CCM na serikali.
Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Jackson Msome, naye alielezea kusikitishwa juu ya unyama uliofanywa na watu hao wasiofahamika.
Hata hivyo Mkuu huyo wa wilaya aliwataka wananchi kushirikiana na polisi kuhakikisha kuwa wauaji hao wanapatikana na kufikishwa katika vyombo vya sheria.Habari zilizopatikana baadaye zilisema tayari polisi wanawashikilia watu wanne wakihusishwa na mauaji hayo ya kikatili.

0 comments