Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA LEO - Obama aonyesha cheti chake cha kuzaliwa

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter

Ikulu ya White House huko Marekani imeonyesha cheti cha kuzaliwa cha Rais Barack Obama, kukabili uvumi wa muda mrefu kwamba kiongozi huyo hakuzaliwa Marekani.
Awali Bw Obama alikuwa ameonyesha tu cheti kinachothibitisha "alizaliwa akiwa hai" kikibainisha alizaliwa Hawaii.
Lakini wapinzani wake wamekuwa wakisisitiza kuwa Bw Obama alizaliwa Kenya, nchi alikozaliwa baba yake, na hivyo kumfanya asikidhi mojawapo ya vigezo vya kuchaguliwa kuwa rais.
Katika siku za karibuni Donald Trump anayedhaniwa kuwa na nia ya kugombea kupitia chama cha Republican alifufua uvumi huo. White House ikahisi kuna haja ya kulikabili swala hilo na kuumaliza uvumi.

Kuachana na upuuzi

Siku ya Jumatano, Bw Obama alielezea hatua hiyo isiyo ya kawaida inalenga kukomesha siasa zisizokuwa na maana, na kusema kwa miaka kadhaa amekuwa akitizama na kuchekeshwa na fitna za kuwa hakuzaliwa Marekani.
"Hatuna muda wa upuuzi wa aina hii," Bw Obama alisema. "Tuna mambo ya muhimu zaidi kufanya. Nina mambo ya maana zaidi kufanya. Tuna matatizo ya kutatua lakini tutayashughulikia, siyo swala hili."
Kutolewa kwa nakala hiyo ya cheti halisi cha Bw Obama, ambacho kilikuwa kimehifadhiwa kwenye chumba maalum chenye usalama huko Hawaii tangu kuzaliwa kwake Agosti 1961, kumetokea baada ya miaka mingi ya uzushi kutoka kwa watu wa Marekani wanaoegemea siasa za mrengo wa kulia.

0 comments

Post a Comment