NAIBU Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe, ameuomba uongozi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), umpe vipindi ili aweze kutoa mchango wake katika kuboresha taaluma katika chuo hicho.
Dk Mwakyembe alifanya hivyo juzi kufuatia ombi lililotolewa na Profesa Mark Mwandosya, la kuwataka wabunge na mawaziri wenye uwezo na nafasi ya kufundisha, wafanye hivyo.
Mwandosya alimtaka Makamu Mkuu wa Udom, Profesa Idrisa Kikula kutumia nafasi ya wabunge wanapokuwa Dodoma kwa ajili ya vikao vyao, kuwaomba waende kufundisha, ili kupunguza pengo la wahadhiri.
Waziri huyo alisema kwa upande wake, yuko tayari kufundisha katika chuo hicho.Kwa upande wake, Mwakyembe alisema na yeye yuko tayari na kuutaka uongozi wa chuo hicho umpangie vipindi na kwamba ataanza kufundisha Juni mwaka huu wakati Bunge la bajeti, ambapo alisema atakuwa Dodoma kwa muda mrefu.
Dk Mwakyembe ambaye amekuwa akialikwa katika vyuo vikuu kadhaa duaniani kwa ajili ya kutoa mihadhara, ni mtalaamu aliyebobea katika sheria.
Kulingana na maelezo yake, somo hilo ndilo atakalokuwa anafundisha Udom.Makamu Mkuu wa Udom Profesa Kikula, alimwagiza Mkuuu wa Idara ya Mafunzo katika Kitivo cha Sheria kuwasiliana mara moja na Dk Mwakyembe, ili kumpatia ratiba ya namna atakayofundisha.
Kabla ya uteuzi wa nafasi ya Makamu wa rais mwaka jana, Dk Mohamed Bilali alikuwa akifundisha katika chuo hicho.Alikuwa anafundisha Fizikia na wanafunzi walikuwa wanamsifu kwa mbinu za ufundishaji.
Kwa upande wake, Waziri wa Elimu na Mafunzoya Ufundi Dk Shukuru Kawambwa alikemea tabia ya wahadhiri wa vyuo mbalimbali nchini, kuhubiri mambo ya siasa vyuoni badala ya kufundisha.
DkKawambwa alisema tabi hiyo imekuwa ikiota mizizi siku hadi siku baadhi ya wahadhili wamekuwa wakidiriki kufundisha hata kwa kutumia mifano ya EPA,Richmond na Dowans.

0 comments