Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA LEO - Mapigano yazuka upya mjini Abidjan

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Mapigano yameanza tena mjini Abidjan, Ivory Coast, baina ya wafuasi wa Ma-rais wawili wanaopinga. Inaarifiwa wapiganaji wa Alassane Ouattara, wanapanga kusonga mbele kuelekea Ikulu, na wameweka amri ya kutotoka nje mjini Abidjan.


Msemaji wa Umoja wa Mataifa mjini Abidjan, anasema kumetokea majibizano ya bunduki karibu na Ikulu.


Watu wengi wamenasa majumbani mwao bila ya chakula, maji au umeme.


Askari wa kulinda amani kutoka Ufaransa, wameudhibiti uwanja wa ndege, kuchukua nafasi ya askari wa Umoja wa Mataifa.


Kiongozi anayekatalia madarakani, Laurent Gbagbo, bado anadhibiti Televisheni ya Taifa na mapema leo ujumbe uliotangazwa kwenye televisheni hiyo uliwataka Askari wa jeshi la Taifa warejee kwenye mapigano mjini Abidjan.


Msemaji wa serikali ya Outtara amesema kwa sasa Bw.Gbagbo anashikilia kasri ya Rais na nyumba yake, na shughuli yao kuu ni kuondoa pingamizi zilizopo katika maeneo mbalimbali ya mji.


Hata hivyo, mkazi mmoja Abidjan amesema sura inayojitokeza ni ya mchanganyiko wa wapiganaji wa pande zote kuonekana wakizunguka mji.


Kufikia sasa vikosi vya Outtara vimeshindwa kuteka sehemu muhimu walizolenga tangu siku ya Alhamisi. Afisi ya Rais, nyumba na Televisheni ya Taifa pamoja na kambi muhimu za jeshi


Viongozi kadhaa wa kijeshi wa upande wa Gbagbo akiwemo mkuu wa majeshi wamekimbia mapigano, lakini bado vikosi vyake vinayazidi majeshi ya Outtara kwa vifaa vya kijeshi vikiwemo vifaru.


Wakati huo huo, Serikali ya Ufaransa imetangza kuwa inatuma askari 300 zaidi kuongezea idadi iliyoko ya kikosi cha kulinda amani ikiwa pia askari hao wanadhidbiti uwanja wa ndege.

0 comments

Post a Comment