Maandamano Tunisia |
Serikali ya Tunisia imesema inataka kumshtaki aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Zine al-Abidine kwa makosa 18, ikiwemo kuua kwa kukusudia na magendo ya dawa za kulevya.
Waziri wa sheria Lazhar Karoui Chebbi amesema mashtaka hayo ni miongoni mwa 44 yaliyotolewa dhidi ya Bw Ben Ali, familia yake na baadhi ya waliokuwa mawaziri.
Hati ya kimataifa ya kukamatwa kwa Ben Ali inaandaliwa.
Alitolewa mwezi Januari wakati wa maandamano yaliyosababisha hata akakimbia nchi hiyo na kuelekea Saudi Arabia.
Serikali ilisema kwa wakati huo ilikamata wanafamilia 33, wakiripotiwa kushutumiwa kwa kupora mali ya nchi hiyo.
Katika mahojiano ya televisheni ya taifa siku ya Jumatano, Bw Chebbi alisema mashtaka 18 yametayarishwa dhidi ya Bw Ben Ali, ikiwemo "njama ya kulifisidi taifa, kuua kwa kukusudia na kufanya magendo ya dawa za kulevya." liliripoti shirika la habari la taifa la Tap
0 comments