MJUMBE wa Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Kilimanjaro, Paul Makonda, ameitaka sekretarieti ya chombo hicho taifa, ikiongozwa na Kaimu mwenyekiti wake, Benno Malisa ijiuzulu na kuanzisha chama chao cha upinzani.
Baadhi ya watu mkoani Kilimanjaro, wametafsiri kauli hiyo kuwa dalili za anguko la jumuiya hiyo ya CCM.
Makonda ametoa kauli hiyo jana mjini Moshi, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu matamko mbalimbali yanayotolewa na jumuiya hiyo kwa vyombo vya habari.Alisema matamshi hayo yanaonyesha wazi kuwa jumuiya hiyo,imepoteza sifa ya kuwa jumuiya ndani ya Chama Cha Mapinduzi.
Alisema kwa mujibu wa taratibu za ndani ya chama,jumuiya ya vijana inapaswa kutoa mapendekezo tu na si kutoa maagizo na kwamba kinachofanywa na sekretari kwa kinaashiria kuwa uongozi wa jumuiya hiyo umeshindwa kusimamia kazi zake.
Alisema hali hiyo pia inadhihirisha kuwa umoja huo sasa unaendeshwa na mafisadi kwa maslahi yao na si kwa ajili ya kujenga chama."Hii ni dalili ya anguko la UVCCM haiwezekani wao wasimame na kuiagiza halmashauri kuu ya chama au waiagize serikali. Haijawahi kutokea tangu kuanzishwa kwa chama, walipaswa kutoa mapendekezo tena si kupitia kwenye vyombo vya habari bali ni ndani ya chama,"alisema.
Makonda alisema uongozi wa UVCCM ukiongozwa na Malisa na Katibu wake John Shigella, ufanya mbinu za kumuandaa kiongozi wa umoja huo mwaka 2012 na mgombea wa urais wa mwaka 2015.
Alisema kazi hiyo inafanywa kwa msaada mkubwa wa mafisadi."Ni kitendo cha aibu kwa jumuiya kudai kuwa itafanya maandamano nchi nzima kuwapinga waasisi wa chama wanaopingana na mafisadi na hii inaonyesha wazi kuwa uongozi wa jumuiya uko upande wa mafisadi. Kwa nini wasiandamane kupinga malipo ya Dowans na matumizi mabaya ya madaraka," alisisitiza.
Makonda alisema matokeo mabaya ya uchaguzi uliopita katika baadhi ya majimbo, yalitokana na utendaji mbovu wa jumuiya hiyo ambayo imeshindwa kuunganisha vijana na badala yake wamebaki kuwa vibaraka wa mafisadi kwa maslahi yao.
"Vijana wengi wa kitanzania wameona Umoja wa Vijana wa CCM si wao na ndio maana wamekimbilia vyama vya upinzani, wanaona UVCCM ni ya watoto wa vigogo na hii imetokana na uongozi wa UVCCM kushindwa kuwaunganisha vijana kulingana na matabaka yao,"alisema.
Makonda alisema kitendo cha UVCCM kumteua Hussein Bashe kuwa Mwenyekiti wa tume ya kuzunguka mikoani, ili kujua sababu za kushindwa kwenye uchaguzi ni tatizo kwa sababu Bashe mwenyewe ni tatizo ndani ya UVCCM.
Alisema hadi sasa hakuna anejua kama Bashe ni Mtanzania halisi ama la.Makonda puia alipinga kitendo cha umoja huo, kumteua mwanasiasa mkongwe Kingunge Ngombaru Mwiru, kuwa Kamanda wa UVCCM na kwa maelezo kuwa hali ilivyo sasa ndani ya nchi Kingunge hana jipya.
Alisema ni vizuri mkongwe huyo akampumzika kwa sababu muda wake umeisha.Alisema ni kweli kwamba mzee Kingunge amefanya mambo mengi ndani ya chama, lakini kwa hali ya sasa ni vema akapumzika.
Alisema kwasasa hakuna mwenye dhamira ya dhati ya kuleta mabadiliko ndani ya UVCCM na kwamba kinachofanyika viongozi hao kutafuta mtu wa kuwalipa kwa masilahi yao.
Aliongeza kuwa kitendo cha viongozi wa UVCCM kupinga kamati kuu kumrudisha Nape Nnauye kwenye nafasi yake ya awali kimeonyesha kuwa wanatumiwa na baadhi ya viongozi ambao hawataki wapambanaji ndani ya chama.
Alisema kwa sababu UVCCM imeamua kuonyesha wazi wanapambana na wanaopambana na mafisadi ni wazi kuwa umma wa watanzania nao umeelewa kuwa viongozi hao ni vibaraka wa mafisadi wanaowatumia kwa maslahi yao.

0 comments