UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani umekitaka chama hicho kuwatoa kafara baadhi ya viongozi wake ili kuepusha msuguano unaodaiwa kuwepo ndani ya chama hicho kwa sasa.
Kauli hiyo imetolewa jana na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Pwani, Abdallah Ulega, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Baraza la Mkoa uliowashirikisha baadhi ya wenyeviti wa UVCCM wa kutoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara.
Ulega alisema katika kipindi cha hivi karibuni, kumekuwa na kauli mbalimbali kutoka kwa wanachama na baadhi ya viongozi wa chama hicho wakiwemo mawaziri wakuu wastaafu Edward Lowassa na Frederick Sumaye walizodai kuwa zimelenga kukibomoa chama hicho.
“Wapo viongozi waandamizi ndani ya chama chetu ambao kazi yao wao ni kukibomoa chama kwa kutoa kauli zenye uchochezi ndani yake ambazo kimsingi zinahatarisha mshikamano uliopo wakiwemo hawa mawaziri wetu wastaafu,” alisema Ulega.
Alisema Sumaye na Lowassa, anashangazwa kwa nafasi walizokuwa nazo ndani ya nchi wanajitokeza katika vyombo vya habari na kuzungumza mambo ambayo kimsingi walikuwa na uwezo wa kukutana na Rais Jakaya Kikwete moja kwa moja na kumshauri kama waliyaona kuwa ya msingi.
Alisema kama nia ya viongozi hao ni kumchafulia Rais na chama hicho kwa maandalizi yao ya kuwania urais mwaka 2015, ni vyema wakasubiri hadi muda utakapofika wa kufuata utaratibu uliowekwa na CCM.
“Hapo baadaye, amani ya nchi itakapopotea, sisi vijana ndiyo tutaonekana chanzo cha yote na zaidi ndiyo tutakaopelekwa katika mahakama ya kihalifu kwenda kujibu mashitaka, hivyo ili kuepuka hilo ni bora tuanze kuenguana wenyewe mapema ndani ya chama chetu ili kuepuka hayo,” alidai Ulega.
Aidha, alitaka Serikali kuzichukulia kampeni zinazofanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kama uhaini kwa vile zinekuwa zikichochea kutokea kwa mchafuko nchini.

0 comments