WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema, sehemu kubwa ya fedha za Mfuko wa Maendeleo ya Kilimo wilayani (DADPS), hazitumiki kwenye miradi iliyokusudiwa na badala yake zinaliwa na wajanja ambao hawana aibu.
Alisema hayo jana mjini hapa alipokuwa akipokea taarifa ya maendeleo ya Mkoa wa Kagera, ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake ya siku nane, ya kuangalia na kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo ya mkoa huo.
“Fedha zinazotolewa kwenye miradi hii ni nyingi lakini ukubwa wa kazi haulingani na matumizi ya fedha hizo, kuna udanganyifu mkubwa sana, zinaliwa na wajanja wasio waaminifu”, alisema Waziri Pinda.
Alisema mfano kwa mwaka wa fedha 2010/2011 Mkoa wa Kagera pekee umetengewa fedha karibu Sh bilioni 10, kwenye mfuko huo na kuwataka watendaji kuwa waangalifu na matumizi yake.
Katika hatua nyingine,Waziri Pinda amesema Mkoa wa Kagera unahitaji kuangaliwa kwa makini kufahamu kwa nini pato la mwananchi halipandi licha ya kuwa na viashirio vya maendeleo.
Alisema Mkoa wa Kagera ni miongoni mwa mikoa mitano ya mwisho nchini kwa wananchi kuwa na pato dogo, mingine ni Kigoma, Shinyanga, Dodoma na wa mwisho ni Singida.
“Kwa takwimu za hapa Kagera kiwango cha kuzaana kinapanda, wakati kitaifa ni asilimia 2.9 hapa kwenu ni 3.3, lazima tuzungumze kuhusu uzazi wa mpango”, alisisitiza Waziri Pinda.
Akizungumzia suala la kilimo, Waziri Pinda alisema ni lazima wananchi waondokane na kilimo cha mkono kwani hakina faida, na kujikita kwenye kilimo cha matrekta.
Alisema kilimo cha mkono hakiwezi kumnufaisha mkulima na akatoa rai kwa watendaji kuwa makini na wasambazaji wa ruzuku za pembejeo kwani kuna mtandao mbovu wa ukiukwaji wa matumizi.
Waziri Pinda jana jioni aliendelea na ziara yake ambapo anatarajia kuwa na mkutano wa hadhara na wananchi katika Uwanja wa Mayunga.

0 comments