Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Maombi ya Mikopo ya elimu ya juu HELSB sasa kwa njia ya mtandao (Online)

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imeanzisha utaratibu mpya wa kuomba mikopo ya Wanafunzi wa elimu ya juu kwa njia ya mtandao yaani “Online Loan Application System (OLAS)”. Mfumo huo mpya utaanza kutumiwa na waombaji mikopo wa mara ya kwanza na Wanafunzi wanaoendelea na masomo kwa mwaka wa masomo 2011/2012. Uombaji mikopo kwa njia ya mtandao umeanzishwa kwa lengo la kuboresha utoaji mikopo na kuimarisha utunzaji wa kumbukumbu za wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu.


Kupitia mfumo huu (OLAS), waombaji wataingiza taarifa zao binafsi na kuziwasilisha Bodi kwa njia ya mtandao. Waombaji mikopo watatakiwa kutembelea tovuti ya Bodi: http://www.heslb.go.tz na kubofya kiunganishi kinachoitwa “Online Loan Application System”. Aidha, Waombaji wanaweza kwenda moja kwa moja katika mfumo wa uombaji mikopo kwa njia ya mtandao kwa anuani ifuatayo http://olas.heslb.go.tz .


Mwongozo unaoelezea jinsi ya kuomba mikopo kupitia mtandao (OLAS) unapatikana katika tovuti ya Bodi. Aidha, Vipeperushi vimesambazwa nchi nzima ili kuwafikia wale wanaotarajia kujiunga na elimu ya juu, Wazazi na Umma kwa ujumla ili kuwaelimisha juu ya utaratibu huu mpya. Vipeperushi hivyo vitapatikana kuanzia tarehe 1 Aprili, 2011 kwenye sehemu zifuatazo: (1) Kwenye Vyuo vya Elimu ya Juu (2) Kwenye Ofisi za Elimu za Wilaya (3) Kwenye matawi yote ya Posta.


Wanafunzi wote wanaotarajia kujiunga na taasisi za elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2011/2012 wanashauriwa kusoma kwa makini mwongozo wa uombaji mikopo ili kupata ufahamu wa zoezi hili hasa jinsi ya kuingia katika mtandao na kuwasilisha fomu za maombi. Ni muhimu kwa waombaji kuwasilisha taarifa sahihi na za kweli ili kuwezesha upangaji wa madaraja ya mikopo kwa waombaji wanaostahili kufanyika kwa ufanisi.


Maombi ya mikopo yataanza kupokelewa rasmi tarehe 1 Aprili, 2011 and tarehe ya mwisho ya kupokea maombi hayo kwa mtandao ni 30 Juni, 2011. Hakutakuwa na muda wa nyongeza baada ya tarehe hiyo kupita.


Kwa masharti na namna ya kujaza fomu za kuombea mkopo
Kama una tatizo lolote ama unapenda kupata taarifa zaidi, usisite kuwasiliana na:


Mkurugenzi Mtendaji,


Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu,


Jengo la TIRDO, Barabara ya Kimweri, Msasani


S.L.P. 76068, Dar es Salaam, Tanzania.


Simu +255 22 2669036/2669037 Faksi: +255 22 2669039


Barua pepe: info@heslb.go.tz


Tovuti: www.heslb.go.tz
Tags:

0 comments

Post a Comment