SIKU moja baada ya wachungaji 32 kutoa tamko la kumkataa Askofu Boniface Kwangu wa Kanisa la
Anglikana Tanzania, Dayosisi ya Victoria Nyanza, ameibuka na kusema hatojiuzulu na kwamba
yuko tayari kukutana na wachungaji hao ili kutafuta suluhu ya mgogoro wao.
Akizungumza na Mwananchi jana kwa njia ya simu,Askofu huyo ambaye yuko safarini mkoani
Morogoro, alisema atakutana na wachungaji ili kutafuta suluhu nje ya vyombo vya habari.
Baraza la Sinodi la kanisa hilo, Novemba 18, 2007 lilimchagua Askofu Boniface Kwangu kuwa askofu
ikiwa ni miezi tisa tu baada ya aliyekuwa Askofu wa Dayosisi hiyo, John Changae kuondolowa
Machi 15, 2007 kutokana na kukataliwa na waumini na wachungaji kwa madai ya kutumia mali za kanisa
vibaya na kujilimbikizia mali za mradi wa kanisa hilo.
Wakati askofu huyo akieleza nia ya kukutana na wachungaji hao, Katibu Mkuu wa Kanisa la Anglikana
Tanzania Profesa Dickson Kilungani alisema ofisi yake inafuatilia kwa kina tamko hilo ili kuona uwezekano wa kutatua mgogoro huo.
Awali akizungumzia mgogoro huo Askofu Kwangu alisema haoni sababu ya kujiuzulu kutokana na madai
anayotuhumiwa nayo na kwamba wachungaji waliosoma tamko la kumkataa siyo watumishi wa dayosisi hiyo na
kwamba walishaondolewa katika kanisa hilo.
“Wananituhumu kuwa nimebadili katiba siyo kweli, mie nimekuta mabadiliko yameshafanyika, sasa mie
nimebadilisha nini, wanalalamika tu wao hawako katika utaratibu, wanapiga kelele za kuleta machafuko,”
alisema Akofu huyo.
“Kwa sasa niko Morogoro, nikirudi Mwanza nitakutana nao ili kuwasikiliza, wanasema nini na madai yao ni nini,
lakini nataka tu watambue kuwa mie sijakataa kukutana nao na madai kwamba sijawahi kuhudhuria vikao vya
usuluhishi, siyo ya kweli, nilihudhuria.” alifafanua Askofu huyo.
Profesa Kilungani akizungumzia mgogoro huo alisema ofisi yake imeupokea kwa masikitiko
makubwa na sasa inasubiri nakala ya tamko la wachungaji hao ili kuona namna kuushughulikia.
Alisema mgogoro wa kanisa hilo Dayosisi ya Victoria Nyanza umekuwa ni wa muda mrefu na
kwamba ofisi yake iliushughulikia mara kadhaa ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua, lakini iwapo wachungaji hao walikuwa hawajaridhika na hatua zilizochukuliwa basi walipaswa kuwasiliana
tena na ofisi yake.
“Mwanza imekuwa na mgogoro wa muda mrefu, kuna hatua ambazo tulichukua na kama hawakuridhika,
wangeendelea kufuatilia na siyo kwenda magazetini, kwa sasa ninaomba nisiseme lolote mpaka hapo
nitaakapopata hilo tamko lao na kulipitia,” alisisitiza katibu huyo.
Katika hatua nyingine, Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Dk Valentino Mokiwa alisema
kuwa hatambui kuwapo kwa mgogoro huo katika Dayosisi ya Vicrotia Nyanza na kusema ameusikia
katika vyombo vya habari.
“Sijui nizungumzie nini, maana leo ndiyo nasikia kuwapo kwa mgogoro kutoka kwako, unaniambia wanasema
kuwa walilalamika kwangu, sijui walileta kwa njia ipi, labda ya posta, lakini kwangu hayajafika,” alifafanua
zaidi Askofu Mokiwa.
Katika tamko lao wachugaji hao ambalo lilisomwa na Mchungaji Marco Iseke mbele ya wachungaji wenzake,
walidai kuwa wameamua kumkataa Askofu huyo kwa madai kwamba ameshindwa kuongoza, ikiwa ni
pamoja na kutumia vibaya fedha na mali za kanisa.

0 comments