Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - 'Kuna matumaini makubwa ya tiba ya Ukimwi karibuni'

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter

WANASAYANSI bingwa wa ugonjwa wa Ukimwi zaidi ya 30 duniani wamekutana Marekani na kubainisha kuwa juhudi za kisayansi zilizofikiwa sasa zinatoa matumaini makubwa ya kupatikana kwa tiba ya ugonjwa huo.

Ukimwi ni ugonjwa ambao unaathiri kinga za binadamu kujikinga na maradhi na umekuwa tishio kwa uchumi hasa katika nchi maskini kwa sababu wengi wa wanaoathirika ni vijana na wataalamu wa fani mbalimbali.

Lakini wanasayansi hao waliokutana mapema wiki hii, Mjini Boston, Marekani walisema kwamba tafiti mbalimbali walizozifanya zimewezesha kupatikana kwa dawa za kupunguza makali ya ugonjwa huo.Kwa sababu hiyo, wanasayansi hao chini ya chama chao cha Kimataifa cha Ukimwi na Jamii (IAS) wana matumaini kwamba miaka michache ijayo kuna uwezekano wa kuwa na tiba yenye uhakika zaidi kuliko ilivyo sasa.

“Chini ya IAS, wanasayansi wanasimamia utafiti wa kisayansi wenye matarajio ya tiba kamili ya Ukimwi,” alisea Profesa Françoise Barre-Sinoussi ambaye alisimamia mkutano huo akiwa mwenyekiti katika taarifa ya mkutano huo iliyototumwa kwa gazeti hili wiki hii.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mkutano huo ulikuwa muhimu kwa wanasayansi hao kuijulisha dunia juu ya maendeleo yaliyofikiwa na hata kuelimisha juu ya mapambano dhidi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU).

Mbali na Profesa Barré-Sinoussi, wataalamu wengine waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na Rais wa IAS, Nobel Laureate; Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Afya Marekani (NIH), Dk Jack Whitescarver na Profesa Steve Deeks wa Chuo Kikuu cha California, San Francisco (UCSF) ambaye pia ni Msimamizi wa Programu ya Wanaoishi na VVU katika hospitali ya San Francisco.

Katika taarifa hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa IAS, Dk Bertrand Audoin alisema kipaumbele cha kwanza cha chama hicho ni kuhimiza mkakati wa kupatikana kwa dawa ya Ukimwi katika kipindi cha mwaka 2010/2014.

“Lengo letu kubwa ni kuhamasisha wataalamu kuwekeza nguvu zao zaidi katika kupata tiba katika kipindi hiki kifupi,” alisema Dk Audoin wakati akielezea mikakati ya IAS.

Akielezea mafanikio yaliyofikiwa na wataalamu hao hadi sasa alisema wamepata dawa za kudhibiti virusi vya ukimwi kuushambulia mwili ingawa bado vinaendelea kubakia mwilini akisema hayo ni mafanikio makubwa katika kupambana na VVU ambavyo viligunduliwa katika maabara mwanzoni mwa miaka ya 1980 na kusababisha mamilioni ya watu kupoteza maisha kutokana na kutokuwa na tiba wala chanjo.

Dk Audoin alisema baada ya mafanikio hayo kwa sasa wanasayansi hao wako mbinu kupata dawa ambayo itawezesha VVU kuangamizwa kabisa kwenye mwili wa binadamu.Kwa mujibu wa taarifa za kisayansi, dawa zaidi ya nane za chanjo zipo kwenye majaribio ingawa wanasayansi wamekataa kuweka wazi siku ambayo watakamilisha kazi hiyo.

Hata hivyo, wanasayansi wanasema kuwa dawa yoyote inapokuwa kwenye majaribio ni vigumu kujua kipindi kitakachotumika kwa sababu kwenye mkachakato huo uboreshaji huweza kufanyika.

Mojawapo ya dawa iliyopo kwenye majaribio ni ya watafiti wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Kuambukiza na Mzio (Niaid) ya Marekani ambayo iligundua chembechembe kinga zinazoweza kidhibiti VVU kwa asilimia 90.

Tags:

0 comments

Post a Comment