Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Utata wa Umeya Arusha, Madiwani wa CHADEMA nao watoka Nje ya Kikao

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
sakata la uchaguzi wa umeya mkoani Arusha limeendelea kukufukuta kufuatia madiwani wa Chadema kususia kikao cha kwanza cha baraza la madiwani wa Manispaa ya Arusha kwa kutoka nje ya ukumbi, kwa madai kwamba hawamtambui meya wa manispaa ya hiyo,  Gaudence Lyimo.

Hatua ya madiwani hao imekuja saa 48 tangu wabunge wa Chadema watoke nje ya bunge ikiwa ni hatua ya kupinga hatua ya kufanyiwa tafsiri maneno ‘Kambi rasmi ya upinzani bungeni’, katika kanuni za bunge toleo la mwaka 2007.

Hatua ya madiwani hao wa Chadema kutoka nje ya ukumbi wakati kikao cha kwanza cha baraza la madiwani kikiendelea kilijitokeza jana majira ya saa 8:30 mchana wakati ajenda ya kuteua kamati za kudumu za manispaa ya Arusha ikitaka kuanza.

Kabla ya madiwani hao kutoka nje kulikuwa na mvutano na malumbano ndani ya kikao hicho baina ya madiwani wa Chadema na CCM hali iliyomlazimisha Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Estomihi Chang’a  kutoka nje ya ukumbi ili kupisha kikao kisicho rasmi cha muafaka baina ya pande hizo, huku mkuu wa wilaya ya Arusha akihudhuria kikao hicho.

Madiwani hao wa Chadema wakiongozwa na kiongozi wao,ambaye ni diwani wa kata ya Elerai, John Bayo walitoka nje na kuwaacha madwiani wa CCM wakiwemo watumishi wakiendelea na kikao.

Akizungumza mara baada ya kutoka nje, Bayo alisema walichukua hatua hiyo baada ya kufikia maafikiano na uongozi wa chama chao ngazi ya taifa ya kuwa hawamtambui meya wa manispaa ya Arusha.

“Sisi hatumtambui meya wa Arusha kwasababu alipatikana kwa njia za zisizo halali, hivyo tumetoka nje ya ukumbi kwa maafikiano ya madiwani wetu na uongozi wa taifa kuwa hatuwezi kushiriki kikao cha utekelezaji na mtu ambaye hatumtabui,"alisema Bayo.

Bayo alisema wao walipokea taarifa za kikao hicho cha madiwani ambapo ajenda walizoambiwa kuwa ni pamoja ana kufungua kikao, kuunda kamati za kudumu za manispaa ya Arusha na kuunda ratiba ya vikao vya manispaa kwa mwaka mzima.

Alisema walipofika katika ukumbi huo waliomba watumishi wa manispaa hiyo watoke nje ili waweze kujadili muafaka wa masuala mbalimbali baina yao na madiwani wa CCM na ndipo walipokubaliana na kisha kuzungumzia masuala mbalimbali walioafikiana baina ya pande zote mbili.

Alidai kuwa mojawapo ya masuala ambayo walikubaliana na madiwani wa CCM ni pamoja na kuitaka serikali izikutanishe pande mbili zinazopingana ili ziweze kujadili hali ya mvutano uliopo na kutafuta suluhu.

Hatahivyo, alisitiza kuwa mara baada ya kikao hicho walikubaliana pia kutafuta muafaka wa suluhu la utata wa umeya wa Arusha lakini baadhi ya madiwani wa CCM walipinga na kudai kuwa waendelee na ajenda zilizopo na suala hilo litafuata baadaye kitendo ambacho hawakukiafiki.

Bayo alisema mbali na kulalamikia uchaguzi wa umeya pia walikuwa na wasiwasi na baadhi ya uundwaji wa kamati za kudumu za manispaa hiyo, kufuatia majina ya madiwani wa Chadema kuwekwa katika orodha katika baadhi ya kamati ihali hawakuomba kamati hizo.

Kwa upande wake Meya Lyimo alisema wanashangazwa na hatua ya madiwani wa Chadema kutoka nje ya kikao hicho kwa madai ya kutotambua nafasi yake.

Lyimo, alidai kuwa pamoja na madiwani hao kususia kikao, wao waliendelea na uundaji wa kamati za kudumu za manispaa ya Arusha kama kawaida bila kuwashirikisha madiwani wa Chadema kwa kuwa hawakuwepo na wataendelea kuchapa kazi za kuwatumikia wananchi.

“Sisi hatukuwafukuza kwenye kikao lakini tumechagua kamati  bila wao kuwepo kwa sababu hawakuwepo pia lakini tulitaka hata wao waongoze baadhi ya kamati,” alisema Lyimo.
Tags:

0 comments

Post a Comment