MWENYEKITI wa Kamati ya Bunge ya Nishari na Madini, January Makamba, amesema yeye na wajumbe wenzake wa kamati hiyo wamejizatiti kuchukua hatua za haraka za kuishauri na ikibidi kuishinikiza serikali kuchukua hatua za haraka na sahihi za kukabiliana na tatizo kubwa la mgawo wa umeme linalolikabili taifa.
January aliyasema hayo jana jioni wakati alipozungumza kwa simu na Tanzania Daima muda mfupi baada ya kuwaongoza wajumbe wa kamati yake kutembelea bwawa la Mtera ambalo ni moja ya vyanzo muhimu vya uzalishaji wa umeme.
“Wakati tukitambua kwamba kazi ya utekelezaji ni ya serikali, baada ya kutembelea Mtera tumemweleza Waziri (wa Nishati na Madini) bayana kwamba tutaishauri serikali na wakati mwingine tutalazimika kuishinikiza kuchukua hatua sahihi na za haraka za kulimaliza tatizo la umeme ambalo lina athari kubwa kwa maendeleo ya taifa,” alisema January.
Katika kuonyesha namna hali ilivyo mbaya alisema hivi sasa Mtera imebakiza kina cha maji cha mita 1.32 tu kabla ya mitambo kuzimwa kutokana na kina cha maji kupungua.
Alisema hali hiyo ndiyo ambayo inalifanya bwawa hilo ambalo lina uwezo wa kuzalisha megawati 80 za umeme litoe megawati 52 tu kwa sasa wakati taifa likisubiri kudra za Mungu kuifanya mvua inyeshe ili kina cha maji kiongezeke.
Akieleza kile walichokiona Mtera, January alisema wamejifunza kwamba ni jambo la hatari kuendelea kuweka matumaini ya kudumu katika umeme unaozalishwa kwa nguvu ya maji wakati hali ikijulikana bayana kwamba mvua ni za msimu na zisizo za uhakika.
January ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bumbuli (CCM), alisema ni jambo lisiloingia akilini kwa taifa kuendelea kuweka matumaini makubwa kwa umeme unaozalishwa na maji yayotokana na kudra za Mwenyezi Mungu za kuleta mvua.
“Leo hii tumekuwa tukiwahimiza wakulima kutumia njia mbadala za kilimo badala ya kuendelea kutegemea mvua iwapo wanataka kupiga hatua. Iweje sisi wenyewe tunaosema hivyo ndiyo tuwe wale wale tunaotaka umeme wetu uwe wa uhakika kwa kutegemea mvua?” alihoji January.
Alisema baada ya kuzungumza na wataalam wa TANESCO wakati wakiwa Mtera, wanajipanga kusafiri hadi Dar es Salaam baada ya vikao vya Bunge kwisha na kukutana nao kujadili kwa kina namna ya kumaliza tatizo la mgawo wa umeme.
Mbunge huyo kijana ambaye ameingia bungeni kwa mara ya kwanza, alisema kamati yake imewaagiza wataalam wa TANESCO kuandaa ripoti ya kina kuhusu hali ya uzalishaji wa umeme nchini ambayo wataijadili wakati watakapokuwa Dar es Salaam.
Alisema tatizo la umeme ni tatizo linalopaswa kutafutiwa ufumbuzi wa haraka kwani hivi sasa imefikia hatua kwamba vyanzo vyote vya kuzalisha umeme wa maji vyenye uwezo wa kutoa megawati 561 vinazalisha megawati 180 tu.
Akiendelea kufafanua alisema vyanzo vingine mbadala vinavyojumuisha umeme unaozalishwa kwa mafuta, gesi, upepo na makaa ya mawe vinaweza kutoa megawati 445 wakati hivi sasa kiasi kinachopatikana ni megawati 290 tu.
January alisema katika hali kama hii ambayo umeme unaozalishwa katika gridi ya taifa ni asilimia 67 tu ya mahitaji yote, haiwezekani mambo yakaachwa yaendelee hivi hivi pasipo hatua za dharura kuchukuliwa.
Akitoa mfano wa aina ya hatua wanazokusudia kuchukua, alisema yeye na wajumbe wenzake wa Kamati ya Nishati na Madini hawawezi kukaa kimya na kuuacha utaratibu wa watu kuagiza jenereta moja kwa muda mrefu uendelee wakati taifa likiumia kiuchumi.
Alisema kwa namna mambo yalivyo serikali inapaswa kuwa tayari kutoa pesa kwa ajili ya kuwekeza katika sekta ya nishati iwapo kweli tuna nia ya dhati ya kukabiliana na tatizo la umeme.
Katika hili alisema serikali inapaswa kujipanga na kwenda mbele zaidi kwa kuwekeza katika miradi endelevu ya umeme na siyo kutafuta mbinu za kukabiliana na tatizo hili kwa mfumo wa kuangalia dharura.
Akitoa mfano alisema matumaini ya haraka ya kupatikana kwa mtambo wa kulinusuru taifa sasa ni yale ya Desemba mwaka huu, muda aliosema ni mbali na ambao hauwezi kulinusuru taifa kwa mahitaji ya sasa.
Akizungumza mara baada ya wabunge kukagua bwawa hilo, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngelej, alisema hali ya mitambo ya uzalishaji umeme nchini si nzuri kutokana na vyanzo vya uzalishaji umeme hasa mabwawa kupungua kwa kiasi kikubwa.
Ngeleja katika maelezo yake hayo alisema madai kwamba tope ndizo zimekuwa zikipunguza uwezo wa mitambo ya Mtera si ya kweli.
“Ili matope yajae kwenye bwawa hili na kuathiri uzalishaji wa umeme inahitaji mkusanyiko wa matope kwa miaka 100; nawaomba waandishi wa habari mtusaidie kuieleza jamii juu ya suala hili… hawa ni wataalam wamesema hivyo,” alisisitiza waziri huyo.
Naye Meneja Mwandamizi wa Uzalishaji Umeme wa Maji wa Shirika la Umeme (TANESCO), Lewanga Tesha, alisema kwa sasa kati ya megawati 1006 zilizokuwa zikizalishwa ni megawati 470 pekee ndizo zinazozalishwa.
Alisema bwawa la Mtera kina chake cha maji kimeshuka na kufikia mita 691.32 juu ya usawa wa bahari ikiwa ni mita 1.32 juu ya kina cha chini ambacho ni mita 690 hivyo kutishia mtambo huo kuzimwa iwapo maji hayo yatazidi kupungua hali ambayo pia ipo kwenye mabwawa mengine.
“Megawati hizi 470 zinazozalishwa kwa sasa zinatokana na upungufu wa maji katika mitambo ya maji kutokana na kuwapo kwa tatizo la mvua pamoja na mitambo mingine na kusababisha kuwapo upungufu wa megawati 230 katika gridi ya taifa,” alisema Tesha.
Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO, Semindu Pawa, aliwataka Watanzania kuvumilia kipindi hiki kigumu cha mgawo na kubainisha hakuna lelemama kwenye kutafuta suluhu ya kudumu ya tatizo la nishati hiyo.

0 comments