Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Chadema watoa msaada wathirika wa mabomu

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
CHADEMA kimetoa msaada wa Mshuka 166 na dawa zenye thamani ya Sh 676,000, kuwasaidia wathirika wa mabomu, yaliotokea hivi karibuni   Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam.

Msaada huo,  una thamani ya Sh 1,676,000, ilitolewa jana  na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willbrod Slaa alipokuwa akitembelea waathirika wa mabomu katika hosptali za jijini Dar es Salaam na eneo la Gongo la Mboto.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam Dk Slaa alisema Chadema imetoa msaada huo, baada ya kubaini msaada wanaopaswa kutoa kwa waathirika hao.

“Tuliambiwa kulikuwa na upungufu wa mashuka 166 na pia dawa, tumekuja na dawa maalumu pamoja na kiasi hicho cha Sh 1 milioni, kwa ajili ya kununua mashuka na kuyawasilisha kwa waathirika,”alisema Dk Slaa.

Katika hatua nyingine Dk Slaa alisema mlipuko wa mabomu ni janga la kuskitisha na kuitaka jamii ya Watanzania kutoliingiza kwenye malumbano na badala yake, wawasaidie waathirika hao, ili warejee maisha ya kawaida.

“Nimetembelea hodi na kujionea mwenyewe namna watu walivyoathirika na mlipuko wa mabomu, wapo kinamama, kinababa na watoto, kwakweli inasikitisha sana, na tukio hili linamfanya mtu akose cha kusema, lakini nasema tu, jali haina kinga.

”alisema Dk Slaa na kuongeza

“Nawaomba Watanzania kwa umoja wetu, kutoingiza suala hili, kwenye malumbano na badala yake, tutumie muda huu, kuwasaidia waathirika warejee kwenye hali ya kawaida.

Katika msafara huo, ambao Dk Slaa aliongozana na wabunge wa Chadema pamoja na viongozi wake wa Mkoa wa Dar es Salaam na Makao makuu, alitembelea katika Hosptali za Amana na  Gongo la Mboto ambako alibainisha kuwa, tukio hilo ni msiba mkubwa kwa taifa la Tanzania.

“Tukio hili, limepoteza maisha ya Watanzania wenzetu na kupunguza nguvu kazi ya taifa, huu ni msiba mkubwa ambao Watanzania hatupaswi kutumia muda hu kwa malumbano bali kujitolea kuwasaidia waathirika hao,”alisisitiza  Dk Slaa.
Awali Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Christopher Mzava alisema hadi kufikia jana Hosptali hiyo, ilikuwa na Majeruhi 27 kati ya 255 waliofikishwa hospitalini hapo, siku ya tukio.

Alisema majeruhi walipo ni wanawake 21, watoto watatu na wanawake watatu na kubainisha kuwa wote wanaendelea vizuri.
Mzava alisema siku ya tukio, walipolea majeruhi 255, maiti za watu 12 na baadaye alifariki mtu mmoja, hivyo kufikia idadi ya maiti 13 na kwamba maiti wote walipelekwa katika Hosptali ya Taifa ya  Muhimbili.
Tags:

0 comments

Post a Comment