Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Profesa: Uwekezaji uko chini ya asilimia 10

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
MHADHIRI wa Chuo Kikuu cha Ushirika na Biashara Moshi (MUCCoBS), Profesa Suleiman Chambo, amebainisha kuwa uwekezaji katika sekta ya kilimo na usafirishaji uko chini ya asilimia 10 ya malengo ya Milenia.







Profesa Chambo alibainisha hayo mwishoni mwa wiki katika kongamano la kujadili historia ya ushirika na umuhimu wa kutunza nyaraka za ushirika, lililohudhuriwa na wadau wa ushirika, wakiwemo viongozi wa vyama vya msingi.






Alisema ingawa malengo ya milenia ni asilimia 10, lakini hivi sasa kilimo ni asilimia tano na usafirishaji ni asilimia tatu. Kongamano hilo, lililoudhuriwa na washiriki 120 na kufanyika katika ukumbi wa Sokoine wa MUCCoBS.






Kadhalika Profesa Chambo ambaye ni mkuu wa zamani wa chuo cha MUCCoBS kabla ya kustaafu aliitaja kikwazo kingine katika ukuaji wa sekta ya ushirika kwamba dhana ya kilimo kwanza imewalenga wakulima wakubwa badala ya wakulima wadogo.






“Inavyoonekana kilimo kwanza ni mkakati wa kitaifa kwa ujenzi wa wakulima wakubwa, wakulima wadogo na ushirika havitamkwi waziwazi na mfumo wa kutoa taarifa za kiuchumi kitaifa uko kimya kuhusu mchango wa ushirika,”alisema.






Profesa Chambo aliishauri serikali iunde mfumo wa kibepari wa kitaifa na unaojitegemea unaowajenga mabepari wakubwa, wa kati na wadogo na wawekezaji wa nje watakiwa kuwa na washiriki wa ndani ya nchi.






“Mfumo huu utazalisha aina mpya ya maamuzi ya kisiasa na kiuchumi katika kujenga uchumi endelevu unaojitegemea wenyewe na kusisitiza kuwa mkakati wa kiushirika unahitajika badala ya kusubiri serikali wakati wote.






Profesa Chambo alifafanua kuwa mustakabili wa sekta ya ushirika unapaswa kuingizwa kwenye mijadala ya kitaifa, ikiwemo katika mjadala wa sasa wa katiba mpya kwa kutoa fursa ya kuainisha mfumo na falsafa ya uchumi.






Kwa upande wake,Naibu mkuu wa chuo hicho, (Utawala),Profesa Leo Donge alisema juhudi kubwa za kukuza na kuendeleza ushirika nchini, zinakwamishwa na ukosefu wa wataalamu wenye uzoefu
Tags:

0 comments

Post a Comment