Viongozi wa kisiasa wanaohasimiana nchini Cote d'Ivoire, Laurent Gbagbo na Alassane Ouattara, wamekubali kufanya mkutano wa ana kwa ana kujaribu kutatua mzozo wa kisiasa nchini humo.
Akizungumza kwa njia ya simu na shirika la habari la AFP kutoka mjini Abuja. mpatanishi wa mzozo huo, ambaye anauwakilisha Umoja wa Afrika, AU, Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga, amesema leo kwamba hatimaye viongozi hao wamekubali kukutana, lakini kwa masharti.
Bwana Odinga ameyasema hayo muda mfupi kabla ya yeye na wapatanishi wanzake wengine watatu kutoka Jumuia ya Kiuchumi ya Afrika magharibi, ECOWAS, kukutana na kiongozi wa sasa wa jumuia hiyo na Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan, ili kumpa taarifa ya ziara yao huko Cote d'Ivoire.
Aidha bwana Odinga amesema mazungumzo yao mjini Abidjan na pande zinazopingana yalikuwa ni mwanzo mzuri na kwamba juhudi zaidi zinahitajika kuweza kupatikana amani nchini humo.
0 comments