Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Mofisa wa kukagua na kudhibiti hesabu za serikali kutinga Udom leo

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter MAOFISA kutoka ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) nchini, leo wanaanza kazi ya kuchunguza malalamiko ya malipo  ya Wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM) na matumizi ya fedha za utawala.
 
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Ludovick Utouh akizungumza na waandishi wa habari jana mara baada ya kufunguliwa mafunzo ya wakaguzi wa hesabu za serikali mjini hapa, alisema tayari maofisa wa ofisi yake walianza kazi jana.
 
Hatua hiyo, imekuja siku moja tu tangu, Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipotembelea chuo hicho, ambacho kimekumbwa na migogoro  na kupokea malalamiko ya wahadhiri wa chuo hicho juu ya malipo ya mishahara yao na pia malalamiko ya matumizi ya fedha yasiyoridhisha  katika chuo hicho
 
" Baada ya kupata maagizo kutoka kwa Waziri Mkuu, leo(jana) maofisa wangu  wameanza kukusanya taarifa Wizara ya elimu , Hazina na  Kamisheni ya vyuo vikuu kabla ya kesho(leo) kwenda Dodoma"alisema Otouh.
 
Otouh alisema baada ya kukamilisha kazi hiyo, watatoa taarifa serikali ili hatua zichukuliwe ili kuhakikisha Chuo Kikuu cha Dodoma kinakuwa shwari.
 
"lengo la serikali ni kuona amani na utulivu vinakuwepo UDOM kwani chuo hiki ni muhimu sana kwa Taifa letu "alisema Utouh.
 
Awali. akifungua mafunzo ya wiki moja ya wakaguzi wa hesabu za serikali, Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Raymond Mushi, aliwataka wataalamu hao kutumia mafunzo watakayopata  kuboresha utendaji wao wa kazi.
 
"Mafunzo haya ni muhimu sana kwenu katika kuwajengea uwezo wa kukusanya ushahidi wa kujua thamani ya fedha katika matumizi na uandishi wa ripoti za ukaguzi"alisema Mushi.
 
Naye Utouh alisema mafunzo hayo ni sehemu ya program ya kuwajengea uwezo wakaguzi wa hesabu za serikali kwa ushirikiano na  mkaguzi mkuu wa nchini Canada.
 
Alisema kupitia taasisi ya  CCAF ya Canada, wakaguzi wa hesabu za serikali, wamekuwa wakipatiwa elimu na pia kupata fursa ya kwenda nchini Canada katika Jimbo la   New Brunwick kujifunza kwa vitendo.

Tags:

0 comments

Post a Comment