KATIBU Mkuu wa CCM, Yusuph Makamba, amesema kuwa na uelewa finyu wa biblia si jambo la ajabu kwake kwa sababu yeye siyo askofu. Makamba aliliambia Mwananchi jana kwa simu, kuwa licha ya uelewa finyu wa biblia, lakini amekuwa akitoa vifungu hivyo kwenye biblia. Makamba alisema hayo kufuatia, Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Thomas Laizer kusema Makamba ana uelewa finyu wa biblia. Laizer alisema hayo juzi mjini Arusha wakati wa kuwaaga watu wawili waliofariki kwa kupigwa risasi na polisi katika maandamano na Chadema yaliyofanyika Januari 5 mwaka huu. “ Ni kweli ninauelewa finyu wa biblia kwa sababu mimi siyo askofu, hata Qurani naweza kuwa siifahamu vizuri kwa sababu mimi siyo Sheikh, ndiyo maana kila ninachozungumza kuhusu dini hizo nakariri vifungu kutoka katika vitabu hivyo,” alisema. Makamba alisema alimweleza Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, kutoandamana kwa sababu serikali ilipiga marufuku maandamano hayo, wao wakapuuza. Alimtaka Laizer kutoa tafsiri ya kitabu cha Warumi 13 sehemu ya kwanza hadi ya saba, inayosema kuwa kila mtu hana budi kutii serikali inayotawala kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu. Alisema kwa hiyo anayepinga mamlaka inayotawala anapinga chombo kilichowekwa na Mungu na watu wanaoasi hujiletea hukumu. “ Kwa maana watawala hawatishi watu wanaotenda mema bali wale wanaotenda maovu, kama hupendi kuishi kwa kumwogopa mwenye mamlaka basi tenda mema naye atakusifu,” alisema. “ Laizer anieleze ufinyu wangu katika uelewa wa biblia upo wapi ikilinganisha na tukio lililotokea mkoani Arusha,” alisema. |
You Are Here: Home - - Makamba amjibu Askofu Laizer
IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
Comments
Hivi Makamba kama msemaji mkuu, anavolumbana na maaskofu anaonyesha busara gani?
Kwa umri na uzoefu wake nilitegemea mawazo ya busara ya kujenga amani, pia angetoa nafasi wenye uchungu na nchi tulumbane kuijenga nchi!
Lkn anachokifanya Makamba ni kuonyesha ubabe wake na CCM, kwamba wamelikusudia kuzuia maendeleo ya democracy kwa hata kwa silaha za moto kama ilivyofanyika Arusha.
Badala ya kuwapa pole waliofiwa CCM kupitia Makamba wanaendeleza mzozo huo akitumia kigezo cha maaskofu, Je mbona Sheikh Alawi alikuwepo kwenye maombolezo? Udini sio tatizo, kwa hiyo CCM isiendeleze chuki za kidini.
Kwa nini Makamba ananukuu kutoka bibilia na sio HUMAN RIGHT ACT? Ama anatufanya wa Tz [NENO BAYA] sio? kama CCM wamesahau wapitia vifungu vya:
-Right to liberty and security
-Freedom of expression
-Freedom of assembly and association
-Prohibition of abuse of rights
-Right to free elections
-Limitation on use of restrictions on rights
Tusishabikie u[NENO BAYA] wa Makamba kutupumbaza na malumbano yake na Maaskofu!
Serikali,CCM na Police wapitie vipengele hivyo vya Human Right Act na watueleze maana ni nini?
UKISIKIA UDINI NDIO HUU SASA
Kennedy usihofu, hiyo ndio advantage kwa wanamageuzi.. udhaifu wa makamba kiutendaji ndio utakaotunufaish a japo damu imemwagika lakini tuvumilie ifikapo 2015 ccm itagundua ilikuwa na wrong person to the wrong position..
Kama kweli ninyi ni wapenda amani na ni wazalendo, na mchango wenu juu ya suala la yupi ni sahihi kati ya Maaskofu au Makamba hautawaliwi na hisia za kidini, ingekuwa VEMA kama mgefanya tafakali ya kina juu ya jambo hili. Na tafakali yenyewe haiwezi kufanywa kwa kuanza kuangalia nyuma yalifanyika yapi.
Sitaki kuamini kuwa Chadema ni CHAMA cha kikristo, wala CUF (maana hoja zenu zinaonyesha kuwa CUF wakifanya jambo, Masheikh ndo wanatetea, na CHADEMA wakifanya, Maaskofu wanatetea). Ninayo mengi ya kuhoji lakini itoshe kujiuliza haya, Nini chimbuko la mgogoro wa Arusha? Nini hoja za msingi zinazolalamikiwa? Je walalamika wanawatuhu maaskofu ama masheikh? Je maandamano yalihusisha wakristo au waislam tu? Waliokufa kwenye maandamano walikuwa wakristo pekee au waislam pekee? Je viongozi wa kidini wa aina zote sio sehemu ya jamii? Na iweje kuhubiri mema bila kukemea maovu?
Chonde watanzania, hii nchi ni yetu sote, likitokea la kutokea haliangalii dini ya mtu, cheo cha mtu wala anakotoka. Acheni kuwa na hisia za udini. Ni mbaya sana!!!