Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Ghasia Tunisia Waziri wa Mambo ya Ndani atimuliwa

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Baada ya ghasia zilizodumu kwa mwezi mmoja nchini Tunisia, Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Mohamed Ghannouchi, ametangaza kumfukuza kazi Waziri wa mambo ya Ndani, Rafik Belhaj, na kuwaachlia huru wale wote waliokamatwa kutokana na ghasia hizo.




Bw Ghannouchi amesema tume itaundwa kuchunguza tuhuma za rushwa nchini humo.


Tangazo hilo limetolewa huku kukiwa na taarifa kwamba wanajeshi wamepelekwa katika mitaa ya mji mkuu wa Tunisia baada ya ghasia kuzuka kwenye baadhi ya maeneo nchini humo.


Ghasia hizo zilizuka wakati wa maandamano ya kupinga ukosefu wa ajira.


Wanachama wa upinzani wamesema takriban watu hamsini wamefariki dunia kufuatia ghasia hizo.


Baadhi ya watu walio katika mji mkuu wa Tunis, wameiambia BBC, wameshuhudia magari ya kijeshi nje ya kituo cha televisheni cha serikali , majengo ya ubalozi na maeneo mengine.


Hatua hii inafuatia mapigano kwenye mji mkuu, baada ya polisi kufyatua risasi hewani ili kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wakiwarushia mawe.


Muungano wa Ulaya umeitaka Serikali ya Tunisia kuacha kutumia nguvu dhidi ya waandamanaji wanaodai ajira na hali bora ya maisha.


Kwenye mji wa Kassarine ambako ghasia zimekithiri, maelfu ya watu bado wanaandamana mitaani wakimtaka Rais Ben Ali, kujiuzulu.


Mtu mmoja aliyeshuhudia, alisema polisi walitoroka na kuwaacha wanajeshi wakilinda majengo muhimu ya usalama.


Maandamano mengine yamepangwa kufanyika siku ya ijumaa.
Tags:

0 comments

Post a Comment