Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Kutengana kwa Sudan Kaskazini na Kusini si vita vya nchi za Magharibi?

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter


Wananchi wa Sudan ya Kusini wameanza kupiga kura ya maoni leo hii ambayo inatarajiwa sana kuamua kujitenga na Sudan ya kaskazini.

 
 Kura hiyo ya maoni ya juma moja ni kipengele muhimu cha makubaliano ya amani ya mwaka 2005 ambayo yamekomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya Waislamu wa kaskazini ya Sudan na Wakristo wa kusini ambavyo vimeuwa watu milioni mbili na kuwapotozea makaazi zaidi ya watu milioni nne.
Kipengee muhimu
Rais wa Sudan kusini Salva Kiir akizuwia machozi yasimtoke wakati wa kupiga kura alitowa heshima zake kwa kiongozi wa zamani wa waasi John Garang ambaye ameuwawa katika ajali ya helikopta hapo mwaka 2005 pamoja na watu wengine waliopoteza maisha yao katika vita.
Muda mfupi baada ya kupiga kura yake katika mji mkuu wa Juba amesema kwamba anaamini Dr. Garang na wale waliokufa pamoja naye watakuwa hawakufa bure.
Kwa Salva Kiir leo ilikuwa ni siku ya kihistoria kwa watu wake.
Watu milioni nne
Wafuasi wa Salva Kiir ,rais wa eneo la Kusini mwa SudanWafuasi wa Salva Kiir ,rais wa eneo la Kusini mwa Sudan
Watu wanaokaribia milioni nne wa kusini wamejiandikisha kupiga kura hiyo ambayo inatakiwa asilimia 60 ya wapiga kura wake washiriki kupiga kura ili iweze kuwa imefanikiwa.
Wengi wanatarajia kuwa wananchi wa Sudan ya kusini watachagua kujitenga na Sudan kusini.
Kulikuwa na misururu mirefu katika vituo vya kupiga kura katika eneo zima la mji wa Juba leo hii na mamia ya watu walilala katika vituo vya kupigia kura katika kituo cha kumbukumbu cha Garang.
Wakati wananchi wa kusini wamejitokeza kwa wingi kupiga kura wale waliojitokeza katika mji mkuu wa Khartoum hawakuwa wengi katika siku hiyo ya kwanza ya kupiga kura.
Hisia za Kaskazini
Wakati wananchi wa kaskazini mwa Sudan hawafurahii kura hiyo kwa kutambua kwamba itaigawa Sudan baadhi ya wananchi wa kusini walioko Khartoum pia wanahisi kwamba watafanywa kuwa wageni huko kaskazini iwapo kusini itajitenga na kaskazini.
Kiongozi mwandamizi wa Sudan kusini leo hii ameionya serikali ya Sudan kaskazini kuheshimu makubaliano juu ya wilaya ya Abyei baada ya kuzuka upya kwa mapigano katika eneo hilo ambapo watu kadhaa waliuwawa na kujeruhiwa hapo jana.

Wanaharakati wanaotaka Sudan ya kusini ijitenge:Sudan ya Kaskazini ina hisia tofautiWanaharakati wanaotaka Sudan ya kusini ijitenge:Sudan ya Kaskazini ina hisia tofauti
Kura hiyo ya maoni ambapo watu wengi walikuwa na wasiwasi iwapo itaweza kufanyika kwa wakati uliopangwa imezusha hofu ya kuibuka upya kwa mzozo kati ya kusini na kaskazini likiwemo suala la Abyei yenye utajiri wa mafuta ambayo inabidi iamuwe iwapo inajiunga na Sudan kaskazini au kusini.
Masuala mengi hayajapatiwa ufumbuzi ikiwemo mipaka ya maeneo yenye akiba kubwa ya mafuta yalioko kusini mwa Sudan.
Tags:

0 comments

Post a Comment