Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Ikulu tano zatikisa kwa ngono. Yupo Raisi wa Marekani

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Mwaka 2010 ambao ulimalizika siku tatu zilizopita, utakumbukwa kwa matukio ya Ikulu tano duniani zikikumbwa na skendo mbalimbali za ngono.

Kwa mujibu skendo hizo, Rais wa Marekani, Barack Hussein Obama ni kiongozi pekee wa kiume ambaye alituhumiwa kumsaliti mkewe wakati kwingineko, wanawake ndiyo waliotajwa kuwaumiza waume zao.

MAREKANI
Rais Obama alituhumiwa kumsaliti mkewe, Michelle kwa kutoka kimapenzi na mwanadada, Vera Baker ambaye ni msaidizi wake wakati wa kampeni za urais mwaka 2008.

AFRIKA KUSINI
Mke wa pili wa Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, Nompumelelo Ntuli alifanya mapenzi na ‘bodigadi’ wake, Phinda Thomo na kupata mimba ambayo ilitoka. Baadaye ilipogundulika, mlinzi huyo alijiua.

SWAZILAND
Mfalme wa Swaziland, Makhosetive Dlamini ‘Mswati III’ alisalitiwa na rafiki yake wa utotoni aliye pia Waziri wa Sheria wa serikali yake, Ndumiso Mamba ambaye alitoka kimapenzi na mmoja wa wakeze, Nothando Dube.

ZIMBABWE
Mke wa Rais Robert Mugabe, Grace alidaiwa kutoka kimapenzi na Gavana wa Benki Kuu wanchi hiyo, Gideon Gono, skendo ambayo imeandikwa mara nyingi na vyombo vya habari vya nchi hiyo.

UFARANSA
Rais wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy alikumbwa na skendo ya kusalitiwa na mke wake, Carla Bruni aliyedaiwa kutoka kimapenzi na mwanamuziki wa nchi hiyo, Benjamin Biolay. 

Hata hivyo, ilidaiwa baadaye Sarkozy alijifariji kwa kutoka kimapenzi na Waziri wa Viumbe na Mazingira wa serikali yake, Chantal Jouanno.
Tags:

0 comments

Post a Comment