KATIKA kuhakikisha vita dhidi ya rushwa nchini inafanikiwa, Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal, amewataka Watanzania kuhakikisha mwaka huu wanafichua viongozi wanaoendekeza vitendo vya rushwa.
Aidha, amewataka viongozi wa dini kuendelea kukemea uozo wa rushwa na mmomonyoko wa maadili kwa jumla, huku akionya kwamba, nguvu ya pamoja isipotumika, kuna hatari ya wananchi kukosa haki zao za msingi.
Dk. Bilal alisema hayo usiku wa kuamkia jana wakati wa Mkesha wa Dua Maalamu kwa Taifa uliofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kwa ajili ya kuuaga mwaka 2010 na kuukaribisha mwaka 2011.
Alisema hatua ya wananchi kushiriki kufichua viongozi wala rushwa, itasaidia kupambana na tatizo sugu la rushwa ambalo ni miongoni mwa matatizo yanayotoa changamoto kwa Serikali kuimarisha amani, utulivu na mshikamano.
"Watu wengi wamekuwa wakihoji upungufu wa maadili miongoni mwa watu wengi, ni kweli kuwa unaotokana na rushwa ambayo ni moja ya changamoto dhidi ya amani, utulivu na mshikamano.
Serikali imedhamiria kwa dhati kupambana na tatizo hilo kwa kuendelea na mikakati madhubuti yenye lengo la kuitokomeza.
Aidha, amewataka viongozi wa dini kuendelea kukemea uozo wa rushwa na mmomonyoko wa maadili kwa jumla, huku akionya kwamba, nguvu ya pamoja isipotumika, kuna hatari ya wananchi kukosa haki zao za msingi. Dk. Bilal alisema hayo usiku wa kuamkia jana wakati wa Mkesha wa Dua Maalamu kwa Taifa uliofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kwa ajili ya kuuaga mwaka 2010 na kuukaribisha mwaka 2011. Alisema hatua ya wananchi kushiriki kufichua viongozi wala rushwa, itasaidia kupambana na tatizo sugu la rushwa ambalo ni miongoni mwa matatizo yanayotoa changamoto kwa Serikali kuimarisha amani, utulivu na mshikamano. "Watu wengi wamekuwa wakihoji upungufu wa maadili miongoni mwa watu wengi, ni kweli kuwa unaotokana na rushwa ambayo ni moja ya changamoto dhidi ya amani, utulivu na mshikamano. Serikali imedhamiria kwa dhati kupambana na tatizo hilo kwa kuendelea na mikakati madhubuti yenye lengo la kuitokomeza. "Rushwa ni adui wa haki, kwani ni tatizo linaloleta dhuluma, uonevu, uhasama, utengano, umasikini miongoni mwa jamii. Zipo sheria za nchi zinazokataza hili, lakini kuondoka kwake kutatokana na kwa kila mmoja wetu kulipiga vita. "Kipindi hiki cha Mwaka Mpya tusipokuwa makini kuna hatari ya wananchi kukosa haki zao, hivyo ni vema wananchi wakafichua viongozi wanaoendeleza rushwa kwa njia mbalimbali." Aliongeza: "Serikali yetu inathamini mchango wa viongozi wa dini wa kukemea rushwa na vitendo viovu vinavyowafanya wananchi kukosa haki na kuhatarisha amani, hivyo endeleeni na mapambano hayo." Akizungumzia umasikini unaowakabili wananchi wengi, alisema Serikali imechukua hatua kadhaa ikiwamo ya kuanzisha mpango wa Mkukuta (wa Kupambana na Kuondoa Umasikini). "Tunazipongeza jumuiya za dini kwa kusaidia kuhamasisha waumini katika jitihada za kuondokana na umasikini kwa kuendesha na kuendeleza miradi ya kujikwamua kimaisha, kwani hakuna njia ya mkato, bali ni kila mmoja kufanya kazi kwa bidii na maarifa." Alikemea pia tabia ya baadhi ya watu kugeuza vyama vingi kuwa mapambano na kujenga chuki na uhasama na utengano kati ya wananchi dhidi ya Serikali na wao wenyewe. Bilal alisema uchaguzi si jambo la mapambano wala si fursa ya watu kujenga na kupandikiza chuki, uhasama na utengano miongoni mwa wananchi au dhidi ya Serikali. Hata hivyo, Bilal ambaye aliingia uwanjani hapo saa 5.30 usiku alitoa mwito kwa Watanzania kujenga utamaduni wa kushindana kwa sera na fikra badala ya kuendeleza chuki, fitna, uhasama na utengano miongoni mwa Watanzania. Mbali na Dar es Salaam pia mkesha kama huo ulifanyika Zanzibar, Kilimanjaro, Arusha, Tabora, Dodoma, Kagera, Ruvuma, Mbeya, Iringa, Tanga, Mwanza na Mtwara. Mwenyekiti wa Taifa wa Kamati ya Maandalizi ya Mkesha huo, Askofu Godfrey Malasi alisema pamoja na Mungu kuibariki Tanzania katika maliasili, lakini imekuwa inakabiliwa na matatizo ya umasikini, rushwa, magonjwa, matendo maovu, kugawanyika kwa familia, uonevu dhidi ya watoto, uchawi, ushirikina, ushoga na usagaji. |
0 comments