MOTO wa malipo kwa Kampuni ya Dowans umezidi kusambaa baada ya Kambi ndogo ya Upinzani bungeni kuonya, kama Serikali ya CCM ikilipa fedha hizo ijiandae kujiuzulu huku Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye, akisema tatizo jambo hilo halikupita kwenye Baraza la Mawaziri. Kambi hiyo ndogo ya upinzani ikitoa tamko ikifananisha Dowans na kashfa ya Goldenberg iliyochangia kuangusha Serikali ya KANU, Kenya, mwenyekiti wa DP Mchungaji Christopher Mtikila, ameibuka na kutoa tamko la kuitisha maandamano nchi nzima kupinga kile alichokiita, "Uporaji wa Nchi kwa Kutumia Bastola ya Dowans.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Sumaye ambaye hii ni mara yake ya kwanza kugusia sakata hilo, alisema tatizo lililopo ni Dowans haijapitia katika baraza la mawaziri na endapo lingeenda katika baraza hilo yasingetokea matatizo hayo.
"Tatizo la Dowans halijaenda kwenye cabinet, (Baraza la Mawaziri), lingeenda kwenye cabinet, nadhani lisingekuwa hivyo," alisema Sumaye.
Sumaye alitoa kauli hiyo nje ya Ukumbi wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), Lugalo ambako alikaribishwa kwenye tafrija ya kuukaribisha mwaka wa 2011 iliyoandaliwa na Umoja wa Maendeleo ya Wakazi wa Wilaya ya Mbulu, Karatu, Babati na Hanang (NORIVADA) waishio Dar es Salaam.
Hata hivyo, Sumaye ambaye hakutaka kabisa kuzungumzia suala la Dowans wala katiba mpya alijikuta akizungumza suala hilo kwa kifupi baada ya waandishi kumbana wakitaka kusikia msimamo wake. Kauli hiyo ya Sumaye iliwahi kutolewa pia na Waziri wa Afrika Mashariki Samuel Sitta, akihoji kutangazwa uamuzi huo bila kupita kwenye ngazi ya Baraza la Mawaziri.
Huku Sumaye akigusia kwa kifupi, kambi hiyo ndogo ya upinzani imetoa tamko katika ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam jana, ambalo Katibu wake David Kafulila, alisema kitendo cha Serikali kutaka kuilipa Dowans kabla suala hilo halijafikishwa bungeni ni sawa na kuchezea moto.
“Chimbuko la Dowans liliangusha Serikali madarakani, hivyo Serikali inatakiwa kutoa nafasi kwa sakata hili kwenda bungeni ili ieleze iweje kampuni ‘batili’ ilipwe kiasi hiki cha fedha,” alifafanua Kafulila, hatua ambayo itaiweka Serikali ya CCM katika ncha ya kisu.
Katibu huyo wa kambi hiyo ndogo, alifafanua kwamba ndani ya Serikali kila kiongozi ana mtazamo wake kuhusu malipo ya Dowans na kusisitiza, suala hilo linatakiwa kuchukuliwa kwa uzito mkubwa.
“Sakata la Dowans Tanzania ni sawa na ‘Goldenberg scandal’ iliyoangusha utawala wa chama cha Kanu nchini Kenya, kashfa hii ilianza mwaka 1993 na kumalizika 2002, Richmond na Dowans ilidumu tangu 2006 hadi sasa hakuna majibu,”alisema Kafulila Kafulila ambaye amewasilisha kusudio lake la kutaka kuwasilisha hoja binafsi bungeni kuhoji sababu zinazoifanya Serikali isiwajibike kwa kuliingizia taifa hasara ya mabilioni ya fedha kwenye sekta ya nishati, alisema Serikali ikipuuza suala la Dowans itapunguza uhalali wake wa kisiasa.
“Pamoja na kuwa kambi hii si rasmi, lakini hatuwezi kukaa kimya katika mambo ya msingi, Dowans ni suala ambalo haliwezi kuzimwa hivi hivi tu wakati ukweli haujajulikana, na kwambia CCM itang’oka madarakani sababu ya Dowans kama ikifanya mchezo, historia ya Kanu itawahukumu,” alisema Kafulila. Aliongeza kwamba, kama CCM hakitang'oka madarakani basi kuna uwezekano nchi ikakumbwa na machafuko.
“Dowans isilipwe mpaka sakata hili lifike bungeni na kupitishwa katika mkaa wa moto wa wabunge, wakilipuuza hili la malipo ya Sh94 bilioni basi wanaweza kupuuza hata malipo feki ya Sh100 bilioni,” alisema Kafulila.
Alifafanua, Dowans ikilipwa kabla ya kujadiliwa bungeni maana yake ni kwamba suala hilo litapanuka na kuongeza kuwa ikiwa hivyo, atawaomba wabunge wapige kura ya kutokuwa na imani na Serikali.
“Hivi hii nguvu na mbio kubwa za kuilipa Dowans zimetoka wapi, mbona malipo ya wastaafu wa EAC na walimu hayapewi kipaumbele, mimi hoja yangu imelenga zaidi hukumu ya ICC kuhusu kulipa Dowans kiasi hiki cha fedha,”alisisitiza Kafulila.
Alipoulizwa kwamba haoni kurudisha sakata la Dowans bungeni linaweza kuibua mengine kuhusu sakata la Richmond ambalo lilisababisha mawaziri kujiuzulu, Kafulila alisema; ...ninachokwenda kuhoji bungeni ni suala la hukumu ya ICC kuilipa Dowans, nataka maelezo katika hilo, najua kuna ambayo hayakusemwa katika ripoti ya Richmond iliyotolewa bungeni na ile kamati ya akina Mwakyembe, inawezekana yakaamka tena, hilo sijui, lakini likiwa hivyo atakayevuliwa nguo chafu na kuvalishwa safi ataonekana.”
Naye Hamad Rashid wakati akizungumzia mwelekeo wa bunge la kumi, alisema kuhusu vurugu zilizotokea Arusha na kusababisha vifo vya watu watatu, Serikali inatakiwa kuboresha mawasiliano kati yake na wananchi ili kuepuka kutokea tukio jingine kama hilo.
“CUF waliwahi kuzuiwa kuandamana, ila taarifa zilikuja usiku, sasa hapo unaweza kuwazuia watu wasiandamane kesho yake, “alihoji Rashid. Akizungumzia uwajibikaji, alisema umefikia wakati wa viongozi wa Serikali kuwajibika na kuongeza kuwa kitendo cha viongozi hao kutowajibika ndio kunakofanya nchi isitulie.
“Kuhusu ushirikiano tumemuandikia Mbowe (Freeman Mbowe) barua Januari 21 mwaka huu kwa kuwa tuliwahi kumweleza kuwa tuko tayari kushirikiana nao ambapo alitujibu kuwa hawezi kuamua suala hilo pekee mpaka maamuzi ya vikao vya chama chake,”alisema Hamad.
Aliongeza, “Tumempa muda wa kutosha na vikao vya chama chake vimeshakaa na kwa kuwa tunaelekea katika vikao vya kumi vya bunge vinaanza Februari 8, tumemtaka atueleze kama jambo la kushirikiana kati yetu na wao litawezekana na hatimaye tufanye kazi kwa pamoja tukiamini kuwa umoja ni agenda ya umma,”alisema Hamad.
Kuhusu mtizamo wa kamati hiyo kuhusu katiba, Hamad alisema umefikia wakati wa Watanzania kuwa na katiba yao ambao wameshiriki kuitunga. “Watanzania waulizwe wanataka mfumo gani wa Serikali, mfumo lazima uwekwe na wananchi kwa kuwa hata tukiwa na rais mwizi basi ashindwe kuiba kwa kuwa atabanwa na mfumo uliopo,”alisema Hamad.
Mtikila aishangaa CC kutaka Dowans ilipwe Kwa upande wake Mtikila alisema, "hii si siasa. Kama CCM ingekuwa inazungumzia kulipa pesa zake tungeruhusu wakae kwenye Nec au CC na kuvaa nguo zao za kijani, lakini hizi ni pesa za umma." Mtikila alisema kulipa fedha hizo ni kuhujumu nchi. Kiongozi huyo ambaye pia huongoza Kanisa la Uokovu Kamili, alisema katika kuonyesha hasira za umma, chama chake kwa kushirikiana na wanaharakati, vyama vingine vya siasa, viongozi wa dini zote kitafanya mandamano makubwa kupinga malipo hayo.
"Hili halitakuwa jambo la kusubiri hata hukumu..., moto huu utawaka wakati wowote. Namtahadharisha Jakaya Kikwete (Rais), asichezee kabisa na moto huu mimi mwenyewe ambaye sifi kwa risasi nitakuwa mbele," alionya Mtikila ambaye ameibuka baada ya kimya cha muda mrefu.
Alifafanua kwamba, pesa hizo za kuilipa Dowans zilitajwa ni Sh 186 bilioni na kuongeza, "Lakini baada ya mayowe dhidi ya majambazi hesabu ikapungua na kuwa sh 94 bilioni." Mwanasiasa huyo mwenye historia ya misukosuko ya kutumikia kifungo jela na anayeoongoza kwa kufungua kesi nyingi mahakamani, aliwataka wananchi kutumia Ibara za 27 na 28 za Katiba na kusisitiza, " hata senti moja hatutaporwa na jambazi lolote."
Aliongeza kwamba, Ibara ya 27 (2) inataka raia wazalendo kuendesha uchumi wa taifa kwa makini kama watu ambao ndiyo waamuzi wa hali ya baadaye ya taifa na kuhoji, "Taifa linauziwa bidhaa gani na Dowans kwa mabilioni ya fedha zetu hizi adimu?" Kwa msisitizo alisema, "Maandalizi ya kile tulicho nacho ni uboreshaji wa maisha yetu sisi sote milioni 44.
Maandalizi ya watoto wetu wote kwa maisha yao ya baadaye, ujenzi wa miundombinu na misingi imara ya uchumi wetu n.k." Akizungumzia msimamo wa Waziri wa Afrika Mashariki Samuel Sitta na Naibu Waziri wa Ujenzi Dk Harrison Mwakyembe, kupinga malipo hayo, Mtikla aliwaunga mkono akisema wako sahihi.
Tangu kutangazwa uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Kibiashara (ICC Court) hapo Novemba mwaka jana ukiagiza Tanesco kuilipa Dowans, taifa limeingia kwenye mjadala mzito huku baraza la mawaziri nalo likigawanyika.

0 comments