Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - CHADEMA Kuishitaki Serikali ICC, EU?

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeelezea dhamira yake ya kutaka kuishitaki Serikali ya Rais Kikwete katika Mahakama ya Kimataifa inayoshughulikia Makosa ya Jinai (ICC), kutokana na kusababisha mauaji ya raia wasio na hatia yaliyofanywa hivi karibuni na Jeshi la Polisi huko mkoani Arusha.

Pia chama hicho kimepanga kuifikisha na kuishitaki serikali kwenye Jumuiya ya Ulaya, iwapo haitawajibika kumfukuza kazi iwapo atashindwa kujiuzulu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Said Mwema, kutokana na kashfa hiyo.

Aidha, CHADEMA ilisema ushahidi wa wazi unaonyesha mauaji hayo yalikuwa na baraka kutoka kwa viongozi wa ngazi ya juu ya serikali ambao ndio waliomshauri Kamanda Mwema kuzuia maandamano hayo muda mfupi na kusababisha ghasia na mauaji hayo.

Tamko hilo limetolewa juzi wilayani Geita, mkoani Mwanza na Mkurugenzi wa Oganizesheni wa chama hicho, Ignas Karashani, wakati akizungumza na waandishi wa habari kulaani mauaji hayo.

Alisema Januari 5, mwaka huu, Jeshi la Polisi mkoani Arusha lililazimika kuwapiga na kuwaua kwa risasi za moto waandamanaji watatu na wengine kujeruhiwa vibaya, katika maandamano yaliyoitishwa na CHADEMA.

"Tumedhamiria kuishtaki serikali kwenye Mahakama ya Kimataifa ya ICC, pia mashitaka haya tutayafikisha kwenye Jumuiya ya Ulaya iwapo Rais Jakaya Kikwete atashindwa kumfukuza kazi IGP Mwema," alisema.

Aidha, alimuonya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuf Makamba, kuacha mara moja kutoa taarifa za kejeli katika masuala yanayoligusa taifa huku akimfananisha na mtu aliyezeeka ndiyo maana katika tukio la mauaji ya Arusha ameendelea kukejeli.

"CHADEMA hatuwezi kuwa na viongozi wanaochochea ghasia na kuua Watanzania wenzetu…Tunachotaka Serikali ya Rais Kikwete iwajibike kwa mauaji ya Arusha," alisema.



Tags:

0 comments

Post a Comment