Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Arusha: baada ya vurugu, diwani ajiunga na CHADEMA

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Katika mkutano huo, diwani maarufu wa CCM wa kata ya Sombetini, Alfonce Mawazo alitangaza kujiondoa katika chama chake na kujiunga na Chadema kwa kile alichoeleza kuwa amechoshwa na ukatili wa CCM.

Mawazo ambaye alihamia CCM mapema mwaka juzi akitokea TLP alipokuwa pia diwani wa kata hiyo, alisema  amekuwa akiunga mkono sera mbali mbali za Chadema zikiwemo sera binafsi za aliyekuwa mgombea wa Urais wa chama hicho, Dk Willibroad Slaa.

 "Naomba niwaeleze wazi kuwa hata katika uchaguzi mkuu mimi ingawa  nilikuwa mgombea wa udiwani wa CCM, nilimchagua Dk Slaa,"alisema Mawazo.

 Hadi jana jioni vurugu kubwa zilikuwa zinaendelea, huku polisi kadhaa waliokuwa wanawatawanya wananchi, wakipigwa na majengo, kadhaa ya CCM, yaliharibiwa.

Mapambano ya polisi na raia yalilipuka upya yakianzia kwenye mkutano wa NMC pale wananchi walipoonyesha nia ya kwenda polisi kuwakomboa wafuasi wa Chadema waliokamatwa jana mchana wakati wakiandamana.
Polisi wazidiwa, waomba msaada

Katika kile kilichodhihirika kuwa ni polisi kuzidiwa nguvu, kundi la askari liliondoka jana usiku katika chuo cha polisi (CCP) mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro kwenda mjini Arusha kuongeza nguvu za kuwadhibiti Chadema.
Askari hao wanafunzi ni wa awamu ya pili, wakilifuatia kundi la wenzao wanaodaiwa kuwa zaidi ya 50 ambao waliondoka CCP Moshi jana saa 11 alfajiri kwenda mkoani Arusha ambako kulizuka vurugu kubwa huku baadhi ya wananchi wakijeruhiwa.

Tags:

0 comments

Post a Comment