Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Gbagbo huenda akangolewa madarakani

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter


Laurent Gbagbo huenda akalazimika kuishi uhamishoni.
Marekani imetangaza kuwa muda unayoyoma kwa rais wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo, kuondoka madarakani na kumkabidhi madaraka mpinzani wake Alassane Outtara anayetambuliwa na jamii ya kimataifa kuwa ndiye aliyeshinda uchaguzi wa urais uliofanyika nchini humo mwezi uliopita.
Huku vikwazo vya kidiplomasia vikizidi kutolewa dhidi ya bwana Gbagbo, mjumbe wa marekani katika eneo la Afrika Magharibi, William Fitzgerald, amesema Washington inaandaa kuchukuwa hatua kadhaa ikiwa ni pamoja na kumwekea vikwazo vya usafiri bwana Gbagbo na familia yake pamoja na kufunga akaunti zake zote za benki.
Umoja wa ulaya EU nao vile vile unatathmini kuchukuwa hatua kama hizo dhidi ya bwana Gbagbo.
Bwana Fitzgerald amesema ikiwa mbinu hizo hazitafanya kazi, kuna uwezekano kwa jeshi la umoja wa Afrika litatumwa nchini humo kumng'oa bwana Gbagbo madarakani kwa lazima.
Amesema anafahamu nchini moja ya kiafrika ambayo imejitolea kumpa hifadhi ya kisiasa bwana Gbagbo ingawa hakuitaja.
Tags:

0 comments

Post a Comment