Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Dowans chungu kwa Mwanasheria Werema, ATAKIWA KUJIUZULU

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter

AG frederick Werema 
MSIMAMO wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema alioutoa juzi kwamba serikali inatakiwa kuilipa kampuni ya kufua umeme ya Dowans Tanzania Ltd fidia ya Sh 185 bilioni umepingwa vikali na baadhi ya wasomi, wanazuoni na wanasaisa nchini. 
Kadhalika baadhi ya watu wa makundi hayo tofauti waliozungumza na Mwananchi jana walisema Jaji Werema hana mamlaka ya kutangaza kufungwa kwa mjadala, huku wakihoji ni nani aliyempa mamlaka hayo na kwamba ana maslahi gani katika kampuni ya Dowans.

Ulipaji wa fidia hiyo unafuatia uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Biashara (ICC Court), Novemba 15, mwaka huu chini ya Mwenyekiti Gerald Aksen na wasuluhishi Swithin Munyantwali, Jonathan Parker ukiamuru Tanesco iilipe Dowans kiasi hicho cha fedha.

Akizungumza na Mwananchi juzi katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kuapishwa kwa Jaji Mkuu mpya, Mohamed Chande Othman, Werema alisema mjadala kuhusu Dowans umefungwa rasmi na kwamba hakuna mpango wa serikali kukata rufaa. Kauli hiyo ya Jaji Werema ni kama imefuta ndoto za Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ambalo lilionyesha nia kwamba lingechukua hatua za kukata rufaa baada ya uamuzi wa ICC kusajiliwa rasmi katika Mahakama Kuu nchini.

Kadhalika kauli hiyo ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ina uelekeo wa kupinga na na ile iliyotolewa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliyewaambia wahariri wiki moja iliyopita kwamba kulikuwa na mchakato wa kuangalia uwezekano wa serikali kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo wa ICC.

 Jaji Werema katika maelezo yake alikwenda mbali zaidi akiwabeza wale waliowahi kutoa kauli za kupinga kulipwa kwa Dowans kwa kusema kuwa “Kwa hukumu hii siwezi kusema tutalivalia njuga suala la Dowans maana kwa hukumu hii hata ukiivalia hiyo njuga itafikia mahala njuga hizo zitakatika tu”.

Ni kutokana na kauli hizo tata na nyingine, baadhi ya wananchi wamehoji kile walichokiita utetezi wa Mwanasheria Mkuu kwa kampuni ya Dowans, huku wengine weakidai kwamba huenda ana maslahi katika kampuni hiyo.

Katibu Mkuu Chama cha Chadema, Dr Willbroad Slaa amemtaka Jaji Werema kujiuzulu kutokana na kuweka wazi kwamba serikali itailipa fidia kampuni ya Dowans Tanzania Ltd.  Dk Slaa ambaye aliibua mjadala mzito kuhusu kampuni hiyo katika vikao vya bunge mjini Dodoma wakati akiwa mbunge wa Karatu , jana aliliambia gazeti hili kwamba kauli ya Jaji Werema inaonyesha jinsi Tanzania ilivyo kichwa cha mwendawazimu.  "Dowans wameingia nchini kwa utaratibu ambao mpaka leo haujajulikana na kurithi mitambo ya Richmond, mitambo ambayo tulizungumza sana kwamba imeingia kwa njia za kifisadi," alisema Dk Slaa,  Aliongeza, " Tuhuma za kampuni hii zilikuwa nzito, zimewekwa wazi lakini serikali haijachukua hatua yoyote, kesi hii mpaka imekwenda mahakamani hakuna lolote la kueleweka,".

Alisema kuwa kitendo cha serikali kukubali kuilipa Kampuni ya Dowans kina maana kwamba fedha zitakazolipwa kwa Kampuni hiyo ni za Watanzania na kufafanua kwamba serikali inalipa deni lisilowahusu.  "Kauli ya Jaji Werema inaonyesha kwamba yeye na serikali ni wazembe, utatoaje idhini bila kuchunguza jambo husika, kuliko kutoa kauli hii alitakiwa kujiuzulu tu," alisema Dk Slaa.  "Nchi hii inaendeshwa vibaya, serikali haiko makini inaipeleka Tanzania sehemu mbaya,".  Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Abdallah Safari alisema umefikiwa wakati serikali ikaweka wazi nani ni mmiliki wa Dowans na kuacha kuwaadaa Watanzania.

 " Jaji Werema anashindwa nini kuwataja wamiliki wa Dowans, hapa tatizo liko wapi......., mikataba hii iliyojaa rushwa imeibua mijadala mikubwa nchini, sasa ili kuweka mambo sawa watueleze nani mmiliki wa Dowans na serikali inamlipa nani,' alisema Profesa Safari  Kwa upande wake Mbunge wa Kigoma Kusini kupitia NCCR Mageuzi, David Kafulila ambaye hivi karibuni alitangaza kusudio lake la kupeleka hoja binafsi katika Mkutano wa Pili wa Bunge, Februari mwakani kutaka serikali iwajibike kwa kuliingiza taifa hasara kwenye sekta ya umeme, kutokana na hukumu ya kesi ya Dowans alisema Jaji Werema “hana ubavu wa kufunga hoja ya Dowans”.

"Hili suala mimi nimeshaliwasilisha bungeni bado kupangiwa siku tu ya mjadala, hapo Werema au serikali haiwezi kuzuia mjadala uliopo bungeni," alifafanua Kafulila. Aliongeza, kuwa Jaji Werema hawezi kufunga mjadala wa hasara ya Sh 185 bilioni na kuongeza kwamba ni lazima aeleze uhalali wa kulipa deni hilo wakati tayari ilishaelezwa mkatabahuo ulikuwa batili.  "Serikali imeshindwa kusema hata mmiliki wa Dowans ni nani, sasa inakwenda kumlipa nani, mzimu au, alihoji Kafulila. Alisema ana imani kwamba Spika wa bunge, Anne Makinda atairuhusu hoja yake na kusisitiza kuwa ataweka mambo yote hadharani ili umma wa watanzania ufahamu mbivu na mbichi kwa kuwa hauwezi kuumizwa na madeni kwa mchezo wa serikali dhaifu.

Naye mhadhiri wa chuo hicho katika Shule ya Sayansi ya Siasa na Uongozi wa Umma, Dk Bashiru Ally, alisema inasikitisha kuona mwanasheria mkuu akitoa msimamo kama huo, wakati ofisi yake inahusika na kuisababishia serikali hasara ya bilioni ya fedha kutokana mikata mibovu ambayo serikali imekuwa ikiingia.

 Ally alisema takribani kipindi cha miaka 20, ofisi hiyo imekuwa ikingia mikataba mbalimbali ambayo badala ya kuwa na tija kwa taifa imekuwa ikisababisha hasara za mabilioni ya fedha. “Werema amerithi ofisi inayonuka rushwa, kwa kipindi kifupi tangu akae katika ofisi hiyo, bado hatujaona juhudi zozote za kusafisha uchafu huu, na vizuri Werema mwenyewe anayajua vema haya kwasababu amekulia katika ofisi hiyo siyo mtu kutoka nje,” alieleza Ally. Alisema kupitia ofisi hiyo, kwa muda huo wa miaka 20 sekta ya madini na nishati kupitia mikataba mibovu inayobarikiwa na ofisi hiyo, imeongoza kwa kulisababishia taifa hasara kubwa.

Ally alitaja baadhi ya mikataba hiyo kuwa ni pamoja na ule wa Kaumpuni ya kufua umeme ya IPTL, Richmond, ununuzi wa Rada na Dowans. “Sasa suala siyo kuangalia kama tulipe ama tusilipe hizo fedha kwa Dowans, ikumbukwe katika nafasi yake ofisi ya mwanasheria mkuu lazima nao walihusika kutoa ushauri wakati wa kesi hii, kwa hiyo jambo la msingi kufahamu Tanzania hatujawahi kuwa na mwanasheria wa serikali anayeweza kusimamia maslahi ya umma,” alisema Ally.

Mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia Chadema, Zitto Kabwe yeye alisema wanasiasa lazima wawajibike katika mjadala wa Kampuni ya Dowans kwa kuwa siasa ziliingia kuanzia kutolewa kwa zabuni hadi kuvunjwa kwa mkataba.  Zitto alisema kuwa anaisubiri hoja ya Kafulila kuhusu umeme ili aweze kuzungumzia Dowans na kutoa maoni yake.  "Suala la msingi hapa ni kujua je ni sawa kulipa Dowans? Bunge lilisema mkataba si halali, mahakama imesemaje kuhusu hilo? Bunge lilisema kampuni ni feki, mahakama imesemaje? Alihoji Zitto.

Alisema kuwa Sh 185 bilioni ni fedha nyingi sana kulipa bila kupata majibu hayo kwani fedha hizo zina uwezo wa kuweka lami kwenye barabara ya kimometa 200 kama Manyoni-Tabora.  "Sakata zima lilijaa siasa na ndo maana tuko hapa,"alisema Zitto.

Kauli ya Zitto inaungwa mkono na ile ya Mkurugenzi wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), Dk Benson Bana amesema serikali ikate rufaa,ili kujiridhisha kama kweli kampuni ya Dowans inastahili kulipwa kiasi hicho cha fedha. "Hizi ni fedha za walipakodi, tusikurupuke kulipa kabla hatujajiridhisha bila kuwa na shaka kwamba kampuni ya Dowans inastahili kiasi hicho cha fedha," alisema.

Alisema inasikitisha kuona wananchi wanayumbishwa na viongozi wasiojua madhara ya maamuzi wanayoyachukua. "Baadhi walishangilia wakati mkataba wa Dowans na Tanesco ulipovunjwa, viongozi walitumia nafasi ya kuvunjwa kwa mkataba huo ili kukamilisha malengo yao ya kisiasa, sasa ni zamu ya kodi ya wananchi kulipa deni hilo," alisema.

Naye Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema Makao Makuu Erasto Tumbo alimshukia Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kueleza kuwa mjadala wa Dowas umefungwa kilichobaki kulipa deni hilo akihoji ana maslahi gani na kampuni hiyo. Alisema hoja iliyopombele ya Watanzania kwa sasa ni kujua nani mmiliki wa kampuni na pia kuona serikali inakata rufaa kama alivyowahi kubainishwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

 “Huyu Warema ni nani hata atuambie Watanzaia mjadala huo umefungwa,ana maslahi gani na kampuni ya Dowans, naomba akae kimya awaache Watanzania wamjue mmiliki wa Kampuni hiyo inayotaka kuchota mali za Watanzania”alisema Tumbo.

Imeandaliwa na Fidelis Butahe, Hussein Issa, Boniface Meena, Fredy Azzah, Raymond Kaminyonge  na Geofrey Nyang'oro


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
Last Updated on Wednesday, 29 December 2010 09:19
 

Comments 

 
0#17 nsolelo 2010-12-29 10:51
Nina wasiwasi na huyo spika makinda sijui kama ataruhusu huo mjadala bungeni.kwani naifahamu sana sera yao ya kulindana.pili nina mashaka na uwezo wa warema hajui sheria ni bora ajiuzuru kuepusha hasara.
Quote
 
 
0#16 Mbowe 2010-12-29 10:50
Naomba tutumie busara katika kufanya analysis ya suala hili. Tatizo la watanzania tunatumia siasa kwa kila jambo. Silaa, Sita na wenzao ndio walikuwa mstari wa mbele kusema mkataba uvunjwe sasa matokeo yake ni hayo. Watanzania hasa viongozi wa siasa wanaongea bila ya utafiti. Tanesco ilikataa kuvunja mkataba wabunge walikuja juu, sasa ni haohao wanaolaumu. Sasa wanasema mwanasheria amesema aliyosema katika maoni ya wanasiasa na wasomi sijaona anayetoa analysis nzuri kutuonyesha sisi wananchi wa kawaida AG amekosea wapi. Tusije tukaamuru AG ajiuzuru halafu baadaye tukajikuta tunalipa pesa zaidi yakawa yale yale. Nyie wenye kujua vitu hivi jaribu kuweka siasa na ushabiki kando na kutuelezea nini kinaendelea. Inashangaza kusikia hawa wasomi na wanasiasa wanasema Dawns ni kampuni ya mafisadi kama vile wanajulikana halafu hapo hapo wanataka kujua Dawns ni ya nini. Tatizo wasomi wetu wote wamekuwa wanasiasa wakiegemea upande wa upinzani na hakuna anayetoa analysis iliyokuwa objective hii ni hatari kwa taifa.
Quote
 
 
0#15 SAUTI YA MTU ALIAYE 2010-12-29 10:50
JESUS CHRIST, TANZANIA YETU NINANI ATAYE TUOKOA. MBONA SELIKARI HII IME JAA LAANA, MAKATILI, HAWANA HURUMA HATA UBINADAMU. KAMA HAMUWEZI KUJIHUZURU, KWA MASLAHI YA WATANZANIA. MTAONDOLEWA HAPO KWA MTUTU WA BUNDUKI. NAONA NDICHO KILICHO BAKI HAPA, MAANA VOTE WHICH IS PEOPLES POWER MUMESHINDWA KUIHESHIMU. WAZEE WETU TUNAWAPENDA, LAKIN KABLA HAMUJA TUANGAMIZA KUTOKANA NA UBINAFSI WENU, INABIDI KUCHUKUA HATUA YA KUWAMALIZA KWA NGUVU NA NJIA YOYOTE ITAKAYO FAA KUTUWEKA HURU NA KUTUPA AMANI YA KWELI WATANZANIA. WEREMA NA JAKAYA PLEASE. TUHURUMIENI, WATANZANIA TUMECHOKA SANA KILICHO BAKI NI KUJITOWA MHANGA.
Quote
 
 
0#14 DEUS M 2010-12-29 10:42
hiv serikali inatupeleka wapi, maana kila kukicha ina tuzulia jambo.Hebu mtajeni mmiliki wa DOWANS msituumishe vichwa watanzaina na kutaka kutu pola kodi zetu kwa maslahi ya wachache .Werema acha watanzania watoe mawazo yao huru na sio kuwaziba midomo;Ee Mungu wetu tusaidie maana taifa letu linapoteza dira sasa.
Quote
 
 
0#13 Mpingo 2010-12-29 10:42
Binafsi, naunga mkono wazo la kuitafutia hoja hii njia ya kurejea bungeni. Yapo mambo ya msingi kabisa yaliyoongelewa hapa yanayotakiwa kupa[NENO BAYA] ufafanuzi kabla ya kuendelea na hatua nyingine.

ICC ilitoa hukumu kwa kuzingatia taratibu zake kunapokuwa na migogoro ya aina hiyo. Udhaifu uliokuwepo ni kwa watetezi wa TANESCO/Serikali kushindwa kuweka bayana matatizo mengine yaliyokuwa nyuma ya Dowans/Richmond. lilikuwa jukumu letu. na sio ICC kuonyesha kwamba Dowans ni kampuni hewa iliyorithi mkataba hewa.
Quote
 
 
0#12 DEUS M 2010-12-29 10:36
Hiv serikali hii inatupeleka wapi,maana kila kukicha inatuzulia jambo.Hebu mtajeni mmiliki wa DOWANS sio kutuumisha vichwa watanzania na kutaka kutupola kodi zetu kwa maslahi ya wachache.Welema acha mawazo huru watanzania wayatoe sio kuwaziba mdomo.Ee Mungu wetu saidia taifa letu maana lina kosa mwelekeo sasa.
Quote
 
 
0#11 Mangi Lelo 2010-12-29 10:20
Kuleni mpaka mumalize
Quote
 
 
0#10 LENGAI 2010-12-29 10:16
Serekali ikilipa Dowans hiyo fedha Bilioni 185 Watanzania wote nchi nzima msilipe kodi tuone JK ataendehsha nchi namna gani?.
Hatuwezi kulipa watu tusiowajua majina yao na mikataba yao fedha zote hizo.Serekali itamke majina yao magazetini na kwenye TV kuwa hwa ni watu gani kwa majina na mikataba yao ichapishwe magazetini kila mtu aione.Hakuna kulipa kodi endapo Serekali italipa Dowans. Sasa Watanzania na sisi tuionyeshe Serekali kuwa haiendeshwi kwa ukoo!!
Quote
 
 
+1#9 mwendapole 2010-12-29 09:50
Kweli Tanzania inaliwa na wajanja!
Na hii ndiyo maana wanawekana kwenye madaraka ili waweze kuitafuna inchi wawezavyo. Kwa upande wangu mimi sioni kama kuna watu makini katika serikali ya ccm. Tanzania itaweza kupata maendeleo pindi mageuzi yatashika hatamu.
Quote
 
 
0#8 nguzu 2010-12-29 09:47
Nchi hii tuna magwiji wa sheria wengi sana tena wa umma, kwa nini kesi hii tusiwape wanasheria wetu makini wa UDSM waisimamie? hata kwa nafasi ya kuishauri (consultancy)se rikali mambo ya sheria za mikataba?

Maana wateule hawa hawatusaidii kwa nafasi zao.
NAOMBA MWONGOZO.
Quote
 
 
0#7 PMN 2010-12-29 09:44
Kwa uhakika watanzania tumefikia wakati tunaburuzwa tu bila kufanya maamuzi yetu kama walipa kodi. Mwanasheria Mkuu anastahili kujiuzuru kwani kazi aliyopewa ya kusimamia mambo ya kisheria nchini, imemshinda. Kwanini aendelee na nafasi hiyo??????? Kama hawezi kujiuzuru basi, Rais Kikwete anatakiwa kujisafisha kwa kukatisha mkataba wake, ili awekwe mtu mwingine mwenye ujuzi zaidi wa kusimamia maslahi ya nchi yetu.
Quote
 
 
0#6 stanley phiri 2010-12-29 09:40
Hakuna sababu ya kuficha mmiliki ama wamiliki wa kampuni ya Dowans. Kwani "company memorandum" haitaji wamiliki hao? Na kama ndivyo basi, hapo wananchi hatuna budi kutia shaka na kufungwa kwa mjadala huu.
Quote
 
 
0#5 ROMLI 2010-12-29 09:33
nilifadhaishwa sana na kauli aliyoitoa mwanasheria mkuu wa serikali kwa kuwa inaonesha jinsi alivyo mdhaifu na hana nia njema na tanzania yetu. huyu mtu ni hatari sana kwa kuwa hana mwelekeo wa uelewa. nakumbuka kipindi cha bunge lililopita likijadili kuhusu sheria ya gharama za uchaguzi alichemka tena hata akawa anatoa lugha tata baada ya bunge kumkomalia.sasa anavyosema kuwa lazima dowans walipwe na mjadala umefungwa, tumueleweje?alitakiwa awe mtetezi mpaka wa taifa kama alivyopewa wadhifa wa kilitumikia kama mwanasheria mkuu ili ufanisi wake uonekane. ni aibu kwa mwanasheria mkuu tuodiriki kutoa kauli dhaifu kama hii. Hafai kuitwa mwanasheria mkuu kwa kuwa hata uwezo wa kujenga hoja hana na ni mropokaji mno. Werema hafai kuwa mwanasheria mkuu wa serikali!!!.inashangaza sana na ni aibu kubwa kwa tanzania kumwajiri mtu kama werema kama mwanasheria wake.
Quote
 
 
0#4 kingumbindo 2010-12-29 09:29
tutatatua vipi swala la dowans iwapo anayekula kwa dowans ndiye mwenye
mamlaka ya kumchukulia dowans hatua?
Quote
 
 
0#3 maharage 2010-12-29 09:27
NDIO MJUE TABIA YA CCM NA SERIKALI YAKE NA MWENYEKITI WAKE KUWA VYEO WANPEWA WATU ILI KULINDANA SIO KWA UWEZO WAKE. RAIS ALIMWEKA HAPO ALIPO AKIJUA KUNA KAZI GANI MBELE NI KITU ALICHOKUWA ANAKIJUA. UNAJUA MAFISADI WAKUBWA WANAUJANJA SANA NA WANATIZAMA MBELE. MTAONA ITAKAVYOKUWA BUNGENI, KWASABABU WALIJUA HII HALI ITATOKEA NDIO KISA CHA KUWEKA WATU WAO SEHEMU NYETI. TUSUBIRI TUONE KAMA HUYO MAKINDA ATARUHUSU HILI SWALA LIONGELEWE BUNGENI. KAMA RAIS WENU NI FISADI MNATEGEMEA NINI? SIMNAONA YEYE AJALI KIMYA ANATOA MWANASHERIA MUISLAM NA KUPANDIKIZA MWINGINE YOTE HAYA KWA MASLAHI YAKE. NCHI HAKUNA RAIS MAFISADI WANATAWALA.
Quote
 
Tags:

0 comments

Post a Comment