Wafuasi hao wa Alassane Ouattara mshindi wa uchaguzi wa rais nchini Cote d'Ivoire mwezi uliopita, walikuwa wamepanga maandamano ya amani jana hadi katika makao ya kituo cha kitaifa cha televisheni nchini humo, lakini safari yao ikakatizwa pale maafisa wa usalama waaminifu kwa rais anayewania muhula mwengine,Laurent Gbagbo,walipowavamia.
Machafuko mjini Abidjan:Wafuasi wa wagombea wote wapambanaMsemaji wa Gbagbo amesema waandamanaji 10, na maafisa 10 wa polisi waliuawa katika makabiliano hayo. Shirika la kutetea haki za binadamu Amnesty International limethibitisha kuwa watu tisa waliuawa, ilhali upande wa Ouattara umesema watu 30 walipoteza maisha yao katika machafuko hayo, ambayo ndiyo mabaya kabisa tangu mgogoro huo wa kisiasa kuanza wiki mbili zilizopita kutokana na utata wa matokeo ya uchaguzi.
Mapambano makali
Waasi wa zamani, wanaomuunga mkono Guillaume Soro, chaguo la Ouattara la waziri Mkuu walikabiliana vikali na maafisa hao wa usalama wanaoiunga mkono serikali ya Ouattara katika mji mkuu wa Abidajan, na pia kulikuwa na vita katika mji wa Tiebissou, eneo linaloigawanya Cote d'Ivoire katika pande mbili tangu vile vita vya wenyewe kwa wenye mwaka 2003.
Wafanyakazi wa UN waondoka Abidjan:Marekani nayo imewaagiza wake warejeeBaraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetishia kuwashtaki kwa makosa ya mauaji ya halaiki wanaopanga na kuetekeleza mashambulizi dhidi ya raia wa Cote d'Ivoire.
Wamarekani waondoka
Marekani kwa upande wake imewaagiza baadhi ya wafanyakazi wake katika ubalozi wake kuondoka nchini humo. Wafanyakazi hao ambao sio wa dharura pamoja na familia zao wametakiwa kuondoka kutoka taifa hilo la Magharibi mwa Afrika, na wakati huo huo, serikali ya Marekani pia imewaonya raia wake dhidi ya kuzuru Cote d'Ivoire.
Mjini Washington afisa mmoja wa ngazi ya juu amebashiri kuwa Gbagbo huenda akasalimu amri na kuachana na madaraka kutokana na shinikizo za Jumuiya ya kimataifa. Afisa huyo alisema wanaamini kuwa Gbagbo anasikiliza kwa makini misimamo ya Marekani, Ufaransa, Umoja wa Afrika na Jumuiya ya kiuchumi ya mataifa ya magharibi wa Afrika ECOWAS, misimamo inayomtaka kumpa madaraka Alassane Ouattara mshindi wa uchaguzi wa rais nchini humo.
0 comments