Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Uchaguzi Tanzania haukuwa na "dosari"

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Wachunguzi wa uchaguzi nchini Tanzania wamesema hakuna taarifa yoyote kuu ya dosari iliyojitokeza inayoweza kuathiri matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika siku ya Jumapili.
Uchaguzi Tanzania haukuwa na dosari
Uchaguzi Tanzania haukuwa na dosari
Kiongozi wa jopo la wachunguzi kutoka Jumuiya ya Madola Bw Paul East, amesema uchaguzi huo uliendeshwa vyema ikilinganishwa na ya miaka mitano iliyopita.
Hata hivyo East amesema kuchapishwa kwa matokeo ya uchaguzi huo kumecheleweshwa sana.
Amesema kutokana na kuwepo teknolojia ya kisasa, haipaswi matokeo hayo ya uchaguzi kuchukua siku nne hata tano kuweza kujulikana.
Wakati huo huo Mawaziri kadhaa tayari wamepoteza viti vyao vya ubunge katika uchaguzi huo.
Tags:

0 comments

Post a Comment