IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
Habari njema kwa maeneo ya migogoro ni kuwa shirika lisilo la kiserikali kutoka Uholanzi limeanza kutoa mafunzo kwa panya kuyagundua na kuyafukua mabomu yaliyozikwa ardhini chini ya mradi wa Apopo nchini Tanzania
Panya wadogo kabisa wanaendelea kupewa mafunzo ya kunusa na kugundua mahala palipofukiwa mabomu huko Morogoro nchini Tanzania. Mradi huo wa aina yake uliopewa jina la APOPO ulizinduliwa na shirika lisilo la kiserikali la Uholanzi.
Panya wengine ambao wameshapata mafunzo chini ya mradi kama huo wameshafanikiwa kugundua mabomu yote yaliyokuwa yamefukiwa nchini Msumbiji, jirani wa kusini wa Tanzania. Panya hao ambao wanagundua mabomu kwa kunusa wanasemekana kuwa na maarifa makubwa kabisa ya kugundua mabomu ya chini ya ardhi.
Aidha mradi huo pia umehusika katika aina nyingine ya mafunzo kwa panya aina nyingine ambao wanaweza kugundua maradhi ya kifua kikuu kupitia vidudu maalum katika maabara ,panya hao wanatoa msaada mkubwa katika suala la uchunguzi wa matibabu ya maradhi hayo katika hospitali za Tanzania ambako kiasi kikubwa cha vipimo vya uchunguzi wa damu vinaweza kuaminika kwa asilimia 60 tu.
Mafunzo hayo ya panya wadogo wekundu yanaanza wakati panya ana umri wa wiki nne ambapo wanawekwa katika mazingira ya kuishi na binadamu ili kuwatoa uoga na hofu wanapoona binadamu pamoja na mazingira mapya na baadaye wanafundishwa kusikia mlio fulani ambao unaashiria kuna chakula kimewekwa mahala.
Mara tu baada ya panya hao kugundua hilo na kulielewa barabara wanafundishwa kutofautisha harufu ya mabomu hayo ya chini ya ardhi ya TNT na harufu nyingine. Shughuli nzima inachukua muda wa hadi miezi 9 ambapo sasa panya hao wanaweza kuwa tayari kupelekwa katika maeneo ambako kuna mabomu ya chini ya ardhi na kuyagundua.
Abdullah Mchomvu mkufunzi wa panya hao anasema sio kazi rahisi kuwafunza panya na pia ni kazi inayohitaji subira ya hali ya juu. Anasema mara nyingine anavunjika moyo sana lakini hurudi nyuma na kutambua kwamba anafanya kazi na panya sio binadamu.
Ni kazi ambayo anasema inahusu suala la kuokoa maisha ya binadamu na ndio sababu anaifanya kwa moyo mmoja. Kawaida mitambo maalum ya kugundua mabomu hayo ya ardhini inaweza kugundua mabomu katika ardhi ya mita 200 za mraba kwa siku lakini panya hao wanaifanya shughuli hiyo kwa masaa mawili pakee.
Muasisi wa mradi huo wa Apopo Bart Weetjens anasema kwamba kazi ya kugundua mabomu sio rahisi na pia ni hatari na pia inagharama kubwa. Lakini kwa kutumia panya imekuwa rahisi zaidi. Aidha kuwafunza panya kazi hiyo pia ni rahisi zaidi kuliko kuwafunza mbwa.
Ama kwa upande wa kugundua maradhi ya kifua kikuu panya hao wamekuwa wa msaada mkubwa ambapo kwa mujibu wa Weetjens, panya wanachukua muda wa dakika 10 pekee kunusa sampuli 70 za mate ya wagonjwa katika maabara na kutoa majibu sahihi kabisa. Baadhi ya wakati panya hao hugundua kwamba kuna viini vya maradhi ya kikua kifuu katika mate ambayo daktari amethibitisha hakuna viini hivyo yaani Negativ.
You Are Here: Home - - Tanzania yatoka kwenye tundu! Serikali ithibiti teknolojia ya Kutumia panya kutegua mabomu na kugundua viini vya kifua kikuu
hawana lolote kuna wanalotafuta hawa!