Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Polisi wamsaka Mbowe

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter POLISI wanamtafuta mgombea ubunge wa Jimbo la Hai kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe kwa tuhuma za kumshambulia mwangalizi wa uchaguzi wa ndani kutoka Temco, Nasri Uronu.

Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Lucas Ngh'oboko alisema Mbowe anadaiwa kufanya shambulio hilo kwa madai kwamba mwangalizi huyo ni kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Shambulio hilo lilifanyika saa tisa alasiri katika kituo cha kupigia kura cha Zahanati Lambo katika Kata ya Machame Kaskazini.

Kwa mujibu wa madai ya mashuhuda wa tukio hilo, ambao hawakutaka kutajwa majina, Mbowe alifika katika kituo hicho kuangalia upigaji kura unavyoendelea.

Inadaiwa baada ya kufika katika kituo hicho, alianza kuwakagua wasimamizi waliokuwepo katika kituo hicho na kuanza kumshambulia Uronu kwa madai kuwa ni kada wa CCM.

Inadaiwa Mbowe alisema kuwa mwangalizi huyo ni kada wa CCM kutokana na uhusiano wake na Mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Hai.

Kutokana na tuhuma hizo, Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai mkoani hapa (RCO), Linus Sizumwa na maofisa wengine wa polisi walichelewa kuwasili katika kituo hicho hivyo walipofika tayari Mbowe alikuwa ameshaondoka.
Tags:

0 comments

Post a Comment