Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Chadema yapeta Moshi Mjini

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Jimbo la Moshi Mjini kinaongoza katika matokeo ya awali ya uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani uliofanyika jana nchini kote.

Hata hivyo, maeneo kadhaa ya Jimbo hilo yalitawaliwa na vurugu za hapa na pale jambo lililowalazimisha Polisi wa Kikosi Maalumu cha Kutuliza Ghasia (FFU) kutumia mabomu ya kutoa machozi kutawanya wananchi waliokuwa wamekusanyika vituoni.

Vurugu kubwa zaidi ziliibuka kata ya Kaloleni ambapo mgombea wa CCM, Michael Mwita alikuwa akichuana vikali na mgombea wa Chadema, Shaban Msuya na kukawa na hisia kuwa CCM ilikuwa na mpango wa kuchakachua matokeo.

Katika kata ya Mawenzi, mgombea Urais wa CCM, Jakaya Kikwete aliibuka na kura 408, dhidi ya kura 339 za Dk Wilbroad Slaa wa Chadema huku wagombea wa vyama vingine wakiambulia kati ya kura 0 hadi tatu.
Tags:

0 comments

Post a Comment