Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Kufichuka kwa nyaraka za siri, changamoto kwa viongozi Ujerumani

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter

Kufichuka kwa nyaraka za siri, changamoto kwa viongozi Ujerumani

 

Kufichuliwa kwa karibu nyaraka 92,000 za siri za jeshi la Marekani kuhusiana na hali nchini Afghanistan kunaleta sura ya wazi ya hali ya vita katika jimbo la Hindukush.

 
Kufichuliwa  kwa   karibu  nyaraka  92,000  za  siri   za jeshi  la  Marekani   kuhusiana  na  hali   nchini Afghanistan  sura  ya  vita  katika   jimbo  la  Hundukush inaonekana  wazi  na  pia  kuleta  hali  ya  kuvunjika  moyo. Na  pia  kwasababu  hali   haionyeshi  kimsingi   mambo mapya,  lakini  baada  ya   kufichuka  kwa  nyaraka  hizo za  siri  kuna  hali  mpya, ambayo  ni mjadala  wa  kweli kuhusiana  na  kuwepo  kwa  majeshi  ya  Ujerumani nchini  Afghanistan.
Nyaraka  hizo  za  siri  zilizowekwa  wazi  katika  mtandao wa  internet  zinaleta  vitu  vitano  vya  kutambua, iwapo nyaraka  zote  ni  za  kweli. Ni  lazima  kufanya  utaratibu huu  wa  kuzipunguza. Kwa  kuwa  hakuna  anayejua , iwapo  taarifa  hizo,  za  idara  ya  upelelezi  na  hali iliyotolewa  ni  ya  kweli  na  ya  hivi  sasa. Mtandao  huo wa  Wikileaks  umeweka  wazi , kuwa   kwa  kufichua  siri hizo  unataka  kumalizwa  kwa   haraka  kwa  vita   nchini Afghanistan. Hali  hiyo  iko  karibu,  kwamba  kutokana  na nyaraka  hizo,  kuwekwa  kwa  majeshi  ya  kimataifa kunakoonekana  kuwa  ni  suala  muhimu,  kunapaswa kufikishwa  mwisho.Mwishowe    nyaraka  15,000  ambazo Wikileaks  inazo  hazijawekwa  katika  mtandao  wa internet.
Mambo  hayo  matano  kuhusu  nyaraka  hizo  ni  pamoja na   vita  dhidi  ya  ugaidi, Taliban  na  hali  ya  jeshi  la kimataifa   chini  ya  uongozi  wa  Marekani  nchini Afghanistan    kutostahili  tena  kuwapo.  Wataliban wameimarika  zaidi   na  wana  silaha  nzuri  zaidi   kuliko ilivyokuwa  hapo  kabla. Makomandoo  maalum wanawatafuta  viongozi  wa  ngazi  za  juu  wa   Taliban pamoja  na  viongozi  wa  makundi  yanayoendesha biashara   ya  mihadarati, na   hawa  wanatakiwa  kuuwawa ama  kukamatwa. Maafisa  wa  Afghanistan , polisi  na jeshi  kwa  sasa  wameimarika  zaidi  kuliko  ilivyofikiriwa hapo  kabla,   kutokana  na  kuwapo  watu  wasioweza kazi,  wasaliti  pamoja  na   mafisadi. Pia  idara  ya  ujasusi ya  Pakistan  inawasaidia  mno  Wataliban.
Kwa  kawaida   watu  walikwisha  hisi  hali  kama  hiyo, lakini  hivi  sasa  inaleta  hali  ya  kufadhaisha.  Ujerumani ikiwa  ni  nchi  ya  tatu  kuwa  na  ujumbe  mkubwa  nchini Afghanistan , imo  katika   hali  ya  kujiuliza, na pia  kuwa  na mjadala  wa  wazi  hatimaye.   Siri  inabaki   lakini    bado katika  upande  wa   wale  wanaofahamu  mengi  ya  ndani na  pamoja  na  kila  kilichowekwa  wazi.
Ni  vipi  jeshi  la  Ujerumani   linaweza  kuchukua  hatua  za haraka   kuhusiana  na  hali  ya  kitisho  katika  jimbo  la Kunduz   na  kaskazini  mwa  Afghanistan. Lijiondoe haraka  ama  vikosi  hivyo  hatimaye  sasa  viimarishwe zaidi  pamoja  na  kupewa  silaha  bora  zaidi.  Je  ni kwamba  serikali  ya  Ujerumani  sasa  itakiri  kuwa  mkakati wa  hivi  sasa  wa  ujenzi  mpya  wa  miradi  ya  kijamii, ambayo  raia  wa  nchi  hiyo  hadi  sasa  wameifurahia , imekuwa  ni  kazi  bure?. Je  lengo  la   vita  hivi  ambalo ndio  kiini  cha   kazi  yote  hiyo  inayofanyika ,  la kuwamaliza  Wataliban  na   magaidi   litafupishwa? Waziri wa  mambo  ya  kigeni  wa  Ujerumani  Guido  Westerwelle ambaye   alionekana  kuwa  na  matumaini  makubwa haonekani  tena  kuwa  na  hali  ya  kujua  la  kufanya. Ni lazima  lakini  alieleze wazi   bunge  kwamba   ni  ndoto kufikiria   kuwa  Afghanistan  inaweza   kuimarishwa usalama  wake  ifikapo  mwaka  2014  na  kuachwa  ikiwa katika  hali  ya  utulivu.
Tags:

0 comments

Post a Comment