Marekani yaidhinisha raia wake kuhama
Marekani imetoa idhini kwa familia za maafisa wake wanafanya kazi katika miji inayopakana na Mexico kuondoka.
Uamuzi huo unafuatia mashambulizi yaliyofanywa na makundi ya wafanyabiashara wa dawa za kulevya dhidi ya maafisa wa ubalozi wa marekani na familia zao.
Watu watatu waliuawa wakitoka katika hafla ya ubalozi wa Ciudad Juarez. Rais Obama ameelezea kughadhabishwa kwake na mashambulizi hayo na kuapa kuwa ataendelea kukabiliana na makundi hayo.
Serikali ya Mexico pia imetoa taarifa kulaani mashambulizi hayo. Serikali hiyo pia imeahidi kuchunguza vilivyo visa hivyo na kuchukua hatua dhidi ya waliohusika.
Zaidi ya watu 18,000 wameuawa katika mashambulizi ambayo yamehusishwa na biashara ya mihadarati tangu mwaka wa 2006 nchini Mexico
0 comments