MOSCOW
Nchini Urusi, katika uchaguzi wa kimkoa hapo jana, pamoja na kuongoza, lakini Chama kinachotawala kimeonekana kupungukiwa umaarufu.
Matokeo ya awali yanaonesha kuwa chama cha United Russia Party cha Waziri Mkuu, Vladmir Putin, kinaongoza katika mikoa yote minane, lakini matokeo yanaonesha kuwa ushindi huo ni chini ya 24 asilimia ya ushindi iliyoupata katika uchaguzi uliopita mwaka 2007.
Kupanda kwa gharama ya maisha pamoja na ongezeko la watu wasiyo na ajira ni vitu vilivyochangia kwa chama cha Waziri Mkuu Putin kupata matokeo hayo.
Vyama vya upinzani vimedai kuwa uchaguzi huo ulifanyiwa hila, na kumlaumu Rais Dmirty Medvedev kwa kushindwa kutimiza ahadi yake ya kuwepo kwa uchaguzi huru na wa haki
0 comments