Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Netanyahau arejea Israel na matumaini

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amekamilisha ziara yake nchini Marekani, huku akisema kuwa kuna mafanikio yaliyofikiwa kuhusiana na suala la ujenzi wa makaazi ya walowezi wa Kiyahudi huko Jerusalem Mashariki.
Akizungumza hii leo kabla ya kurejea Israel, bwana Netanyahu amesema kuwa, wamepata njia ambayo itairuhusu Marekani kuendelea na juhudi zake za kuyafufua mazungumzo ya amani ya Mashariki ya Kati, lakini kwa kuheshimu maslahi ya kitaifa ya Israel.
Mjini Amman, Mfalme Abdullah wa pili wa Jordan amesema kuwa mpango wa amani katika eneo hilo uko njia panda, kutokana na hatua ya Israel kutangaza ujenzi wa makaazi hayo ya walowezi.
Ameonya kuwa Israel inacheza na kile alichokiita moto, kwa kuendelea na mpango huo, na kusema kuwa njia zote za kisiasa, kisheria na kidiplomasia bado ziko wazi kuweza kukabiliana na kitendo hicho cha Israel.
Tags:

0 comments

Post a Comment