IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
MAKAO makuu ya Kanisa Katoliki duniani Vatican, jana yalimweka wakfu rasmi Mtanzania wa kwanza Monsinyori Novatus Rugambwa kuwa Balozi wa Baba Mtakatifu na Askofu mkuu katika nchi za Angola na Sao Tome na Principe huku Rais Jakaya Kikwete akituma salamu za pongezi.
Monsinyori Rugambwa amesimikwa kushika daraja la uaskofu jana mchana mjini Vatican katika Ibada ya misa takatifu maalum iliyoongozwa na Mwadhama Kardinali Tarcisio Bertone, Katibu wa Baba Mtakatifu, iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.
Kuwekwa wakfu kwa Askofu monsinyori Rugambwa kuwa balozi katika nchi hizo kunafuatia uteuzi wa kiongozi wa kanisa hilo duniani Papa Benedikto wa XVI, ambapo Rais Kikwete katika salamu zake ameuelezea uteuzi huo kuwa umetokana na utumishi wake uliotukuka kwa kanisa hilo na pia ni heshima kwa Tanzania.
“Baba Askofu, nimepokea kwa furaha nyingi na faraja kubwa habari za uteuzi wako wa kuwa Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki na Balozi wa Papa katika nchi za Angola, na Sao Tome na Principe,†alisema Rais Kikwete katika salamu hizo kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu jana.
Kwa mujibu wa Ikulu Rais Kikwete alisema, “Kwa niaba ya Watanzania wenzako, kwa niaba ya Serikali yangu nami binafsi, napenda kukupongeza sana kwa uteuzi huo. Uteuzi huo ni heshima kwa nchi yako, ni heshima kwa Watanzania wenzako na ni matokeo ya utumishi wako uliotukuka katika Kanisa. Ni nafasi unayoistahili.â€
Aidha katika salamu hizo Rais Kikwete amemtakia Askofu Rugambwa kila la heri katika utumishi wake huo mpya na kumhakikishia kuwa Watanzania wapo pamoja naye katika sala ili Mungu amjalie nguvu na afya njema aweze kumudu nafasi hizo.
You Are Here: Home - - Mtanzania wa kwanza balozi wa Papa Huko Angola na Sao Tome
0 comments