Rais Barack Obama wa Marekani kwa mara nyingine ametoa ujumbe maalum kwa Iran, inayosherehekea mwaka wake mpya mwishoni mwa juma hili.
Amesema mapendekezo ya Marekani la kufanya mazungumzo na ushirikiano na Iran liko pale pale, licha ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili kuzidi kuzorota.
Rais Obama emesema Marekani inataka watu wa Iran wawe na mfumo wa sheria ulio sawa kwa wote, heshima, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kutumia mtandao wa internet kwa ajili ya mawasiliano bila serikali kuingilia au kufuatilia.
Mara tu baada ya kuchaguliwa kuwa Rais, Bw Obama alitoa wito kwa Iran kuwa na mwanzo mpya, lakini tangu wakati huo uhusiano baina ya nchi hizo mbili umezidi kuzorota.
0 comments