Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - EU yaipinga Israel

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Mkuu wa sera za Nje wa Umoja wa Ulaya, Catherine Ashton, amesema uamuzi wa Israel kujenga nyumba mpya za walowezi wa kiyahudi katika maeneo ya waarab huko Jerusalem Mashariki unazikwaza juhudi za kufufuliwa mazungumzo ya amani kwenye eneo la Mashariki ya Kati.
Akizungumza mjini Cairo Misri katika kikao cha Umoja wa nchi za kiarabu, Arab League, Bibi Ashton amesema Umoja wa Ulaya unatilia maanani suala la usalama wa Israel na kuwa unaunga mkono mpango utakaotoa haki, uhuru na heshima kwa Wapalestina.
Amesisitiza kuwa msimamao wa Umoja huo wa Ulaya katika suala la ujenzi wa nyumba hizo uko wazi kabisa, kuwa ni kinyume na sheria, kikwazo kwa amani na unatishia kuweko mataifa mawili kama suluhisho la  mzozo wa eneo hilo.
Bibi Ashton pia anatarajiwa kuizuru Israel pamoja na Ukanda wa Gaza.
Tags:

0 comments

Post a Comment