Kansela wa Ujerumani Angela Merkel aliushutumu uamuzi wa Israel kujenga nyumba mpya za walowezi katika maeneo ya Waarab inayoyakalia kwa nguvu huko Jerusalem Mashariki.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Berlin, mara baada ya mkutano wake na Waziri Mkauu wa Lebanon, Saad Hariri, Kansela Merkel amesema kitendo hicho kinarudisha nyuma kwa kiwango kikubwa juhudi za kupatikana amani ya kudumu huko Mashariki ya Kati.
Pia Kansela Merkel amesema kuwa muda umekaribia kwa Iran kuwekewa vikwazo kutokana na nchi hiyo kukaidi azimio la kuitaka isitishe mpango wake wa nyuklia. Amesisitiza kuwa wanaelekea katika hatua ya kuiwekea vikwazo nchi hiyo.
Kauli yake hiyo imekuja siku moja baada ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Bernard Kouchner, kusema kuwa Umoja wa Ulaya uko tayari kuiwekea vikwazo Iran.
0 comments